Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Huu hapa umuhimu wa kumiliki mali binafsi

Katika maisha ya kila siku, kumiliki mali au vifaa mbalimbali ni jambo la msingi linaloweza kuboresha ustawi wa mtu binafsi na jamii kwa jumla.

Mali zinaweza kuwa na umiliki wa mtu binafsi, serikali na vikundi au mashirika ya biashara na yasiyo ya kibiashara.

Hapa, tutaangalia zaidi mali zinazomilikiwa na mtu binafsi, familia au kaya, hii ikiwa na maana kuwa kaya inaweza kumiliki vitu kama nyumba, gari, vifaa vya kielektroniki, simu, akiba ya fedha au hata mali zisizohamishika kama ardhi.

Kutunza mali katika kaya si tu kwa ajili ya manufaa ya sasa, bali pia ni kwa ajili ya usalama wa kifedha wa baadaye na hapa kila mwanakaya anapaswa kujifunza jinsi ya kuthamini mali zilizopo katika kaya na kuzitumia kwa njia sahihi. Hapa kuna sababu kuu zinazoeleza umuhimu wa kutunza mali kwenye kaya.

Jambo la kwanza Usalama wa Kifedha, moja ya faida kubwa ya kuwa na mali katika kaya ni kutoa usalama wa kifedha, hii ikiwa na maana kuwa kama unamiliki mali kama nyumba, gari au akiba ya fedha, unajihakikishia kuwa na chanzo cha msaada wakati wa dharura.

Kwa mfano, fedha zilizowekwa akiba zinaweza kutumika wakati wa matatizo ya kiafya au dharura nyinginezo, hiyo huondoa mzigo wa kutegemea mikopo au msaada wa haraka kutoka kwa watu wengine.

Vilevile, mali kama nyumba au ardhi zinaweza kutumika kama dhamana ya mikopo kwa ajili ya kuanzisha biashara au miradi mingine ya maendeleo. Hii inasaidia sana kwa watu ambao wanataka kujiongeza kiuchumi kwa kutumia mali zao.

Pia mali ni mtaji, unapokuwa na mali inakuwa na thamani kubwa wakati mwingine kuliko kiasi cha fedha kilichotumika kununulia hiyo mali, hii ikiwa na maana kuwa unaweza usiwe na uwezo wa kununua mali nyingine kama ambayo tayari unamiliki.

Kitu cha pili ni thamani ya muda mrefu. Tofauti na mali nyingine ambazo ni kwa ajili ya matumizi ya kila siku kama vile vifaa vya kielektroniki, mali kama ardhi na nyumba, zina tabia ya kuongeza thamani kadiri muda unavyopita.

Umiliki wa ardhi au nyumba unaweza kuwa ni mali ambazo thamani yake huongezeka kulingana na mahitaji ya soko na maendeleo ya kiuchumi katika eneo husika.

Kwa hiyo, kumiliki ardhi kunamaanisha unajenga thamani ya muda mrefu ambayo inaweza kukuletea faida kubwa siku na kizazi kijacho.

Kitu cha tatu ni uwezo wa kujipatia kipato, baadhi ya mali zinaweza kuwa chanzo cha mapato ya ziada, kwa mfano, nyumba za kupangisha au magari yanayotumika kwa ajili ya biashara ya usafirishaji.

Vitu hivi vinaweza kukuzalishia kipato cha ziada ambacho kitasaidia katika gharama za maisha au hata uwekezaji mwingine.

Unaweza kuwa pia na aina fulani ya mashine au vifaa vya kielektroniki ambavyo unaweza kukodisha kwa ajili ya kuongeza kipato. Mathalani kama unamiliki nyumba ya ziada na kuipangisha pangishaji.

Fedha zinazopatikana katika kodi za pango zinaweza kutumika kuendeleza miradi mingine, kulipa mikopo au hata kuongeza akiba ya kifedha.

Hivyo, unapofikiria kumiliki mali ni vizuri kuangalia lengo la umiliki kama ni kwa ajili ya muda mfupi ama muda mreafu, pia angalia kama unaweza kumudu gharama za kusimamia mali husika