Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wauza simu Kariakoo walizwa na kodi

Muktasari:

Gazeti hili lilifika katika maduka ya simu ya Mtaa wa Msimbazi na Kariakoo na kukuta baadhi yakiwa na simu kidogo wakati zile za gharama kubwa zikiwa chache.

Dar es Salaam. Umakini wa kukusanya kodi unaofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), umeanza kudhoofisha biashara katika baadhi ya maduka ya bidhaa mbalimbali, ikiwamo simu eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Gazeti hili lilifika katika maduka ya simu ya Mtaa wa Msimbazi na Kariakoo na kukuta baadhi yakiwa na simu kidogo wakati zile za gharama kubwa zikiwa chache.

Baadhi ya wauzaji walidai kodi imechangia uhaba huo, kwa kuwa kila kinachoingizwa nchini kwa sasa kinalipiwa.

Mmoja wa wafanyabiashara hao, Agban Singh alisema ni bora kuagiza simu za bei ya kawaida kuliko za gharama kwa sababu wanunuzi hakuna na kodi ni asilimia 100.

“Unajua ni tofauti na zamani. Hivi sasa hakuna mzigo unaopita bila kukatwa (kodi) kitu ambacho kinachangia kuwapo kwa mizigo michache na ya kawaida,” alisema.

Sufiani Khamis aliyekuwa anachukua simu na kuzitembeza kwenye baa na maeneo ya starehe, alisema ameacha kufanya biashara hiyo, badala yake anashinda dukani kwa tajiri yake wakiuza zilizopo kwa sababu mzigo uliopo ni mdogo.

“Si unaona hata mali zilizopo siyo za gharama ni za kawaida, kuagiza simu halisi hivi sasa siyo kitu rahisi, ukileta mzigo uwe umejipanga. Hakuna ujanjaujanja, sijui kama tutaendelea kuagiza mzigo wa maana, ”alisema.

Akbar Yunus alisema wafanyabiashara wengi wadogo walikuwa wanatamba kutokana na kushirikiana na wafanyabiashara wakubwa kuagiza mizigo ‘kimtindo’, lakini sasa kila mtu anayeagiza wa kwake anatakiwa alipie kodi halisi kulingana na mzigo.

“Wengi hawakuwa na mtaji wa kutosha, lakini walikuwapo,” alisema. Yunus.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Walipakodi wa TRA, Richard Kayombo alisema hawajamkataza mfanyabiashara yeyote kuagiza mzigo na wala hawatozi kodi kwa kukomoa, bali kwa kufuata sheria zilizopo.

“Mfanyabiashara anayefanya shughuli zake kwa usahihi hana haja ya kuogopa, ”alisema Kayombo.