Wajumbe kuanza na viti maalumu kesho
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla
Dar es Salaam. Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imeteua makanda mbalimbali katika nafasi za kuwania Ubunge wa Viti Maalumu ambao kesho wataanza kupigiwa kura za maoni.
Uteuzi huo umetangazwa leo Jumanne, Julai 29, 2025 na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla baada ya kumalizika kwa kamati kamati Julai 28, 2025.
Makalla amesema uwepo wa watia nia wengi katika nafasi mbalimbali zilizotangazwa umethibitisha kuwa CCM ni chama pendwa kinachoaminika, kinachotegemewa huku wananchi wakiamini kuwa hatima ya uongozi iko ndani yake.
Kutokana na wingi huo, amewataka wagombea watakaokosa nafasi katika uteuzi wa awali, kuendelea kutoa ushirikiano ndani ya chama.
Kundi hilo la viti maalumu linajumuisha wawakilishi wa mikoa (bara), makundi ya wasomi, wenye ulemavu, wafanyakazi, asasi za kiraia (NGO’s) pamoja na UWT Zanzibar.
Baada ya uteuzi huo leo Julai 30, 2025 mikutano mikuu maalumu ya mikoa ya UWT itaketi kupiga kura ya maoni kwa wagombea wa ubunge wa viti maalumu bara na wagombea ubunge/uwakilishi (Zanzibar).
Agosti mosi, asubuhi kutafanyika mkutano mkuu maalumu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kupiga kura ya maoni kwa wagombea wa ubunge/uwakilishi wa viti maalumu vijana kwa upande wa Zanzibar na Tanzania Bara
Siku hiyo pia, mchana mkutano mkuu maalumu wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Taifa, utafanyika kupiga kura ya maoni kwa wagombea wa ubunge/uwakilishi wa viti maalumu kwa upande wa Zanzibar na Tanzania Bara.
Mkutano huo, utafuatiwa na mkutano mkuu maalumu wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Taifa kupiga kura ya maoni kwa wagombea wa ubunge wa viti maalumu vya makundi (Tanzania Bara) na ubunge/uwakilishi viti maalumu (Zanzibar), Agosti 2, 2025.
Walioteuliwa viti maalumu
Miongoni mwa walioteuliwa kwa Mkoa wa Arusha ni; Lilian Badi, Zaytun Swai, Athuman Issa, Martha Kivunge, Dk Asanterabi Lowassa, Navoi Mollel, Martha Amon na Catheline Magige.
Dar es Salaam walioteuliwa ni, Janeth Maghanga, Neema Kiusa, Doreen Kahwa, Mossy Msindo, Maida Juma, Amina Said, Georgina Lukwembe, Janejelly Ntante na Zainab Janguo.
Mkoa wa Dodoma walioteuliwa ni Asia Abdallah, Raphia Kimaro, Anna Mahendeka, Stellar Mamotto, Jesca Mbogo, Dayana Ngurumo, Salama Nyundo, Joyce Kaishozi na Halima Zuberi.
Geita wameteuliwa Josephine Chagula, Vicky Kamata, Janeth Kasobi, Naomi Maalim, Getruda Manyesha, Catherine Mbumbe, Mwanaidi Shekue na Regina Mkenze.
Mkoa wa Iringa walioteuliwa ni Rose Tweve, Nancy Nyalusi, Fatma Rembo, Seki Kasuga, Tumaini Msowoya, Scola GodsonMbosa, Maria Makombe na Lydia Nzema.
Kwa mkoa Kagera walioteuliwa ni Samira Amour, Devotha Mburarugaba, Anitha Nyamziga, Elizabeth Ngaiza, Evastina Mgata, Anitha Korongo, Anitha Bunono na Herieth Rugaju.
Katavi walioteuliwa ni Martha Mariki, Taska Mbogo, Fortunata Kabeja, Stella Chenchele, Janeth Pinda, Elizabeth Sultani, Angelina Ntemo na Mahija Nyembo.
Kigoma waliopenya ni Zainabu Katimba, Ashura Kahoye, Amina Kaumo, Naomi Mwaipopo, Prisca Mapunda, Sabreena Sungura, Selina Makebe na Jackline Rugo.
Kilimanjaro wamepenya Zuena Bushiri, Regina Chonjo, Esther Malleko, Caroline Lyimo, Pamela Mallya, Never Zekeya, Mary Nashanda na Aika Ngowi.
Katika Lindi waliopitishwa ni Tecla Engele, Maimuna Patham, Riziki Lulida, Zainabu Kawawa na Zena Katambo.
Mkoani Manyara wamepita Regina Qwaray, Yustina Rahhi, Paulina Nahato, Loema Issay, Scola Mollel, Anna Shinini, Jocyelyne Umbula na Senorina Jorojick.
Mara waliopenya ni Agness Marwa, Ghati Chomete, Joyce Mang’o, Neddy Lima, Rhobi Samwelly, Dk Graec Mwangwa, Sophia Marwan na Bingile Washima.
Mbeya ni Suma Fyandomo, Maryprisca Mahundi, Ikupa Mwaifwami, Tumaini Mwakasege, Sara Mwangasa, Hobokela Mwamkina, Anna Mwangolombe na Upendo Kalasa. Mkoa wa Morogoro ni Jane Mihanji, Amina Karuma, Sheila Lukuba, Hajira Mwikoko, Lucy Kombani, Kulwa Kangeta, Aliyah Omar, Rahel Mashishanga na Josephine Kupuna
Mkoa wa Mtwara walioteuliwa ni Agness Hokororo, Dk Ahmed Hingora, Athumin Mapalilo, Daiys Ibrahimu, Jane Chikomo, Asha Motto, Sophia Malandi, Tunza Malapo na Mshhiri Mwanemo.
Mwanza ni Mary Masanja, Kabula Shitobela, Furaha Matondo, Khadija Liganga, Adellah Mayengela, Suzana Kabula, Jesca Wanna na Lidya Miyaye.
Njombe ni Dk Pindi Chana, Neema Mgaya, Rebecca Nsemwa, Scholastika Kevela, Anna Mwalongo, Tegemea Mbogela, Magreth Kyando na Tulalumba Mloge.
Mkoa wa Pwani ni Hawa Chakoma, Mariam Ibarahim, Irene Makongoro, Fatuma Mssumi, Nancy Mutalemwa, Rewhema Issa, Rehema Msemo na Sifa Mwaruka.
Rukwa ni Bupe Mwakang’ata, Anastella Malaji, Agripina Mbalamwezi, Lucy Mwanisawa, Jacqueline Mzindakaya, Agatha Maliyawatu, Sylivia Sigula na Dorice Manyungu.
Ruvuma waloteuliwa ni Jacqueliln Msongozi, Mariam Madalu Nyoka, Happiness Ngwando, Getrude Haule, Laura Hyera, Sabrina Lipukila, Sophia Kihelile na Otilia Hyera.
Katika mkoa wa Shinyanga walioteuliwa ni Santiel Kirumba, Christina Mnzava, Salome Makamba, Christina Gule, Alice Kyanila, Feliter Buzuka, Mwanahamisi Munkunda na Queenelizabeth Makune.
Simiyu wanaokwenda kuumana kwa wajumbe ni Ester Midimu, Minza Mjika, Tinner Chenge, Caritas Machupa, Jane Masanja, Grace Mabula, Rosemary Ngh’wani na Limi Kilalo.
Singida ni Matha Gwau, Aysharose Mattembe, Matha Nduguru, Grace Mkoma, Mwajuma Ngimba, Tatu Ntandu, Fancy Nkuhi na Verediana Lie.
Songwe walioteuliwa ni Juliana Shonza, Neema Mwandabila, Tumaini Mbembela, Neema Lwila, Betha Minga, Messiah Swella,Tully Magilla, Shukuruni Mkonda na Winfrida Shonde
Tabora walioteuliwa ni Aziza Ally, Jaqueline Andrew, Christina Mndeme, Zuena Yusuph, Dk Bayoum Kigwangala, Mkuwe Issale, Rebeka Kashindye na Zahra Michuzi, huku Tanga wakipita ni Husna Sekiboko, Mwanaisha Ulenge, Mwantumu Zodo, Macrina Clement, Kadodo Magadi, Fatuma Shaha, Sharifa Abebe na Mboni Masimba.
Walioteuliwa kugombea nafasi ya ubunge viti maalumu makundi, (wasomi, wenye ulemavu, wafanyakazi na NGO's UWT- Zanzibar kwa kundi la wasomi ameteuliwa Dk Zeyana Abdallah Hamad, Mwanaidi Ali Khamis, Bhai Ibrahim Khamis na Dk Salma Abdi Mahmoud.
Kundi la Wafanyakazi UWT ameteuliwa Tunu Juma Kondo,Kalathumi Kondo Makame, Lucy Edward Mwakyembe na Asha Abdalla Salum.
Kwa kundi la NGO's walioteuliwa ni Saumu Juma Ali, Zuhura Saleh Amour, Mgeni Hassan Juma, Jamila Mahmoud Juma, Anisa Mwinyi Mzee na Mashavu Sukwa Said
Kundi la walemavu walioteuliwa ni Nasriya Nassir Ali,Fatma Djaa Chesa, Siyenu Haji Mkanga, Yumna Mmanga Omar, Jide Khamis Saleh.
Upande wa UVCCM walioteuliwa ni Amina Perera Ame,Kazija Omar Faki,Bimkubwa Iddi Hamad, Raya Mmaka Hamad, Amina Miraj Hassan, Zainab Abdallah Issa
Wengine ni Latifa Khamis Juakali ,Asma Ali Makame, Monica Edward Maziku,Amina Ali Mzee, Zainab Hassan Omar ,Zadida Abdalla Rashid, Salma Mzee Shaaban, Mziu Mkashaa Shaame, Mwanaenzi Hassan Suluhu, Aziza Omar Suwedi na Amina Bakar Yussuf.