Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

UVCCM waitana kwa wingi uchaguzi 2024

Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana Mkoa wa Iringa Agrey Tonga akizungumza na wanachama wa jumuiya hiyo katika majimbo matatu Mafinga Mjini, Mufindi kaskazini pamoja na Mufindi kusini. Picha na Mary Sanyiwa

Muktasari:

  • UVCCM wawataka wananchama wao wenye sifa, uwezo, na nidhamu, kuacha woga na hivyo kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa ifikapo 2024, badala ya kuwaachia wazee.

Mufindi. Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa, wametakiwa kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa ifikapo 2024.

Aitha, vijana hao wametakiwa kutoogopa vitisho vyovyote juu ya nafasi hizo kwani kijana yeyote wenye sifa, uwezo na nidhamu, anafaa kuwa kiongozi.

Hayo yamebainishwa na leo Jumatano  may 3,2023 na  Mwenyekiti wa uvccm Mkoa wa Iringa Agrey Tonga, wakati  wa ziara ya Kamati ya Utekelezaji ya Mkoa, ilipotembea na kuzungumza na vijana wa jumuiya  hiyo, katika majimbo matatu ya Mafinga Mjini, Mufindi kaskazini pamoja na Mufindi kusini.

Aidha Mwenyekiti huyo amesema kuwa haiwezekana kuendelea kuongozwa na wazee ambao kimsingi hawawezi kutembea, wakati vijana wenye uwezo, nidhamu na sifa za kushika nyadhifa hizo wapo, lakini kwa hofu; wamewaachia wazee kuongoza.

"Tunaka vijana ndio washike nafasi hizi huku wazee wakiwa wanatuangalia ili tukikosea waweze kuturekebisha kwa sababu hatuwezi kuwaachia wazee ndio watuongeze hadi wanazeeka  wakati vijana wenye nidhamu na uwezo wapo. Hivyo nawasisite vijana wenzangu tujitokeze kuombea nafasi hizi ifikapo 2024." Amesema Tonga

Naye katibu wa  jumuiya hiyo kata ya Upendo Octavian Mtewa amesema wao kama viongozi wamepokea maagizo hayo kwa sababu walikuwa wanadhani nafasi hizo za uongozi wa Serikali za Mitaa  wazee ndio wanapaswa kugombea pekee.

"Tunashukuru Mwenyekiti wetu wa Mkoa Agrey Tonga kwa elimu ambayo ametupatia, hakika hatutamwangusha  hivyo uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 ategemee vijana tutajitokeza kwa wingi kufika kugombea nafasi hiyo." Amesema Mtewa

Kwa upande wake mwenezi wa Wilaya ya Mufindi Dickson Mtevele maarufu villa, amesema jumuiya  ya vijana ndio ambao wanategemewa  kutoa dira na taswira ya uimara wa Chama cha mapinduzi ( CCM) Wilaya hapa.

"Kwa sasa taifa letu chini ya Mwenyekiti wetu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameruhusu Mikutano ya hadhara, hivyo kama vijana wa Chama msione kan kwamba hatua hii haina nia njema, badala yake tuitumie kama fursa kueleza  mafanikio  ambayo Chama na jumuiya wameyafikia." Amesema Mtevele.