Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

UVCCM Moshi Vijijini waanza safari ya kujitegemea kiuchumi

Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Moshi vijijini, Yuvenal Shirima.

Moshi. Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro, unakusudia kuanzisha kiwanda cha kuzalisha chaki, hatua ambayo itawawezesha kujiendesha na kuondoka kwenye utegemezi.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa UVCCM Moshi vijijini, Yuvenal Shirima wakati akitoa taarifa ya utekelezaji na mafanikio waliyoyapata kama jumuiya katika kipindi cha mwaka mmoja, akisema uanzishaji wa kiwanda hicho, kutachochea ajira kwa vijana na kuinua uchumi.

Shirima amesema mbali na kiwanda cha chaki, wameanza ujenzi wa vyumba vya biashara katika eneo lao lililoko Kata ya Makuyuni wilayani humo na kwamba kukamilika kwake kutainua uchumi wa jumuiya na kuwawezesha kujiendesha.

“Tumeweza kuandaa mpango biashara wa kuanzisha kiwanda cha chaki na mpango wa kuanzisha mradi huu tumeshauandaa na lengo letu ni kuhakikisha tunaukamilisha ili kuweza kujiimarisha kama jumuiya na kuinua vijana kiuchumi,” amesema Shirima.

Shirima amesema mbali na miradi hiyo, katika kipindi cha mwaka mmoja, tayari wameanzisha ujenzi wa nyumba ya mtumishi na jengo la ofisi ya Jumuiya hiyo ambapo yapo katika hatua ya lenta.

Akizungumzia mchango wa jumuiya hiyo kwa jamii, Shirima amesema katika kipindi cha mwaka mmoja cha uongozi wao wameanzisha kampeni ya kuchangia ukarabati wa miundombinu ya madarasa ambapo tayari wamekarabati katika shule tatu ikiwemo Shule ya sekondari ya Himo.

Amesema wanaendelea kuwaunganisha vijana pamoja na kuhakikisha katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu, wanaungana na kuwa wamoja ili kukisaidia chama kupata ushindi wa kishindo.

Kwa upande wake, Katibu wa uhamasishaji na Chipukizi wa jumuiya hiyo Wilaya ya Moshi vijijini, Ally Badi amesema kamati ya utekelezaji imejipanga kuhakikisha jumuiya inakuwa na miradi mbalimbali ya kiuchumi ili kuweza kujitegemea.

“Katika kipindi cha mwaka mmoja tumefanya mambo mengi na pamoja na kuanzisha miradi ya kiuchumi, pia tumeweza kuwaunganisha vijana na kuhamasisha utalii wa ndani,” amesema