Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia: Kuundwa kwa INEC kumejibu kilio cha wadau wa siasa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akihutubia na kuhitimisha shughuli za Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe Juni, 27,2025.

Muktasari:

  • Amesema hatua hiyo imetokana na mapendekezo ya wadau wa demokrasia kupitia Kikosi Kazi alichokiunda kilichokusanya maoni ya wadau wa makundi mbalimbali ikiwemo vya siasa.

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan, amesema kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) kumejibu wa hoja wa wadau wa siasa waliokuwa wakiitaka kwa muda mrefu.

Amesema hatua hiyo imetokana na mapendekezo ya wadau wa demokrasia kupitia Kikosi Kazi alichokiunda kilichokusanya maoni ya wadau wa makundi mbalimbali ikiwemo vya siasa.

Ameeleza hayo leo Ijumaa Juni 27,2025 wakati akihutubia Bunge jijini Dodoma, akihitimisha shughuli za Bunge la 12, ikiwa ni maandalizi ya kwenda katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025.

“Kwa mara kwanza katika historia ya nchi yetu, Tume Huru ya Uchaguzi iliundwa kwa sheria yake yenyewe. Tulifanya hivi ili kujibu rai ya muda mrefu ya wadau wa kisiasa,” amesema Rais Samia.

Mbali na hilo, amesema miongoni mwa maboresho yaliyofanyika katika Sheria ya Uchaguzi ni pamoja kuongeza takwa la mgombea kupigiwa kura ya hapana, hata kama yupo peke yake.

“Hatua hii inafuta kilichojulikana kama anapita bila kupingwa,” amesema Rais Samia.

Mbali na hilo, Rais Samia amesema hivi sasa asasi za kiraia zimekuwa huru kuendesha shughuli zake ili kukukata na kuishawishi Serikali kupitia mapendekezo yao.

Kuhusu mchakato wa Katiba Mpya, Rais Samia amesema ni mojawapo ya ahadi zilizotajwa katika Ilani ya CCM ya mwaka 2025/26, na kwamba utekelezaji wake utafanyika ndani ya miaka mitano ijayo.