Nanghejwa Kaboyoka atimkia ACT Wazalendo

Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu na kada wa zamani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Nanghejwa Kaboyoka amejiunga na Chama cha ACT Wazalendo.
Kaboyoka ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki ametambulishwa leo Jumamosi, Juni 28, 2025 na Kiongozi wa ACT Wazalendo, Dorothy Semu. Huu ni mwendelezo wa waliokuwa wabunge 19 waliofukuzwa uanachama ndani ya Chadema, kujiunga na vyama vingine vya siasa. Tayari Ester Bulaya ametangaza kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Endelea kufuatilia mitandao ya Mwananchi