Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwalimu ataja vigezo wananchi vya kumpima achaguliwe kuwaongoza

Mgombea urais kupitia Chaumma, Salum Mwalim, akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Sandala, Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro, wakati wa ziara yake ya kusaka wadhamini leo Agosti 23, 2025.

Muktasari:

  • Mwalimu awageukia wanaosema umri wake hautoshi kumudu majukum ya urais, asema urais siyo umri.

Hai. Mtiania wa urais wa Tanzania kwa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Salum Mwalimu amesema uongozi haupimwi kwa umri bali kwa uwezo wa akili na hofu ya Mungu..
Mwalimu ameyasema hayo aliposimama kusalimia wananchi wa mji wa Bomang'ombe waliojitokeza barabarani kumlaki akiwa njiani kuelekea Moshi kutoka Arusha.

"Msiniangalie kwa umri wangu, nipimeni kwa uwezo wangu na hofu ya Mungu," amesema na kuongeza;

"Kama uongozi ni umri, tumechagua wazee kwa miaka 60 mambo yamebaki vilevile tu, mwaka huu nichagueni mimi Salum Mwalimu ninawahakikishia sitawaangusha," amesema



Leo, Mwalimu anatarajia kuhitimisha ziara yake mikoani, tangu alipoanza Jumamosi Agosti 16, 2025 akisaka wadhamini katika safari yake kuusaka urais wa Tanzania.