Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makalla ajitoa ugomvi wa Makonda, Gambo

Muktasari:

  • Kwa mara kadhaa kumekuwa na majibizano baina ya Makonda na Gambo, huku chanzo kikihusishwa kuwa ni uchaguzi mkuu, hata hivyo, Makonda hajaweka wazi nia yake ya kuwania ubunge katika jimbo hilo.

Arusha. Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla amesema hawezi kuingilia ugomvi kati ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda na Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo.

Amesema viongozi hao wote ni wadogo zake na ni marafiki, hivyo anawatakia kila la heri katika mchakato unaofuata (ambao hakuutaja).

Makalla amebainisha hayo leo Ijumaa Juni 6, 2025 wakati akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Soko Kuu la Arusha katika ziara yake inayoendelea katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini.

Kwa mara kadhaa kumekuwa na majibizano baina ya Makonda na Gambo, huku chanzo kikihusishwa kuwa ni uchaguzi mkuu, hata hivyo, Makonda hajaweka wazi nia yake ya kuwania ubunge katika jimbo hilo.

“Hawa wote, Gambo na Makonda, nawatakia kila la heri, wote wananifahamu, ni kaka yao, kipindi hiki kidogo mambo siyo mazuri, lakini yatapita na mimi nawatakia kila mmoja kila la heri katika mchakato utakaofuata,” amesema Makalla.

Ameongeza: “Nawatakia kila la heri, wote hawa wananifahamu, ni kaka yao. Gambo alikuwa anasoma Chuo cha Uhasibu, nilikuja hapa akawa mjumbe wa Baraza, Makonda kama alivyoeleza, alikuwa Chuo cha Ushirika. Wote mimi ni kaka yao, na mimi nasimama kuwatakia kila la heri, siwezi kuingilia ugomvi.”

Ameongeza kwamba ukishakuwa na wadogo zako, unawaacha kwani mambo hayo ni madogo na yatapita. Amesisitiza kwamba Gambon a Makonda ni watoto wa mama mmoja na baba mmoja, ambaye CCM.

“Kwanza, ni marafiki, kuweni makini. Hawa ni marafiki, wanajuana, kwa hiyo kipindi hiki kidogo mambo siyo mazuri lakini tutapita na mimi nawatakia kila mmoja wao kila la heri katika mchakato utakaofuata,” amehitimisha.


Makonda na Gambo

Awali, Makonda amesema anashangaa watu wanaoshindwa kutambua mchango wake kama Mkuu wa Mkoa na kuwa ni matatizo ya dakika za majeruhi, lakini ukweli ni kwamba kazi imefanyika na wakibaki peke yao wanakiri “mwamba” yuko kazini.

Makonda amesema miradi mingi katika Jiji la Arusha ilikwama ikawa kero kwa wananchi na kuwa alipofika katika mkoa huo, alianza kuwapiga spana wanaochelewesha utekelezaji wa miradi ili unapofika wakati wa uchaguzi mkuu, Oktoba, mwaka huu, CCM iwe na vitu vya kuonyesha.

Awali, kabla Makonda hajasimama jukwaani, alisimama Gambo ambaye aliwatambua viongozi wengine wote akiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Thomas Ole Sabaya, lakini hakumtaja Makonda.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Makonda amesema wakati mikoa kama Dar es Salaam na Mwanza ikiwa imekamilisha ujenzi wa stendi zake, Jiji la Arusha walikuwa wakipigana majungu na kukwamisha miradi mbalimbali.

“Hapa kulikuwa na miradi mingi sana, ilikwama na ikawa ni kero kwa wananchi na mwisho wa siku wakaanza kuwa na mashaka ya kuahidiwa kila siku kila kukicha ahadi. Mimi nilipofika ahadi yangu ya kwanza, niliwapiga spana wote waliochelewesha miradi,” amesema.

Makonda amesema Serikali imewezesha ujenzi wa miradi mbalimbali iliyokwama ikiwemo ujenzi wa jengo la utawala la Halmashauri ya Jiji la Arusha na kuwa kwa sasa ujenzi huo umefikia asilimia 70 na kuwa amemtaka Mkandarasi kuhakikisha hadi mwisho wa mwezi Julai anakuwa amemamaliza kwa hatua hiyo ya awali ili aanze hatua ya umaliziaji.

“Wakati ukiwa Mkuu wa Mkoa unasimamia ujenzi wa stendi, John Mongela (Naibu Katibu Mkuu CCM Bara) akiwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza alisimamia stendi na mimi nikiwa mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, nilisimamia ujenzi wa stendi ya Magufuli,” amesema.

“Hapa walikuwa wanapiga majungu na ushirikina, hapa ni fitina na ajali nyingi, nimekuja hapa tumepiga spana sasa ujenzi unaendelea na sababu ilikuwa moja tu nilitamani tukienda uchaguzi 2025 CCM iwe na kitu cha kuonyesha,” amesema Makonda ambaye awali alitambulisha viongozi, alimtaja na Gambo.


Gambo azungumzia miradi

Kwa upande wake, Gambo amesema Serikali imetekeleza mradi wa Tactics ikiwemo ujenzi wa masoko ya kisasa ya Kilombero na kwa Morombo, shule mpya za sekondari na msingi.

“Watu wanaosema hakuna kilichofanyika, wanatakiwa kuwekwa chini ili wajue Arusha ilipotoka na inapokwenda, tulipo na tunapokwenda, Makalla nakupongeza unavyojibu mapigo maeneo yenye upotoshaji,” amesema.

Amesema uwanja wa ndege Kisongo hadi Kilombero na mwaka 2021 tulijenga hoja serikali ilikiwa inafanya upembuzi yakinifu ili kulipa fidia, tumepewa taarifa imekamilika, wananchi wanatakiwa kulipwa fidia ya Sh10 bilioni italipwa ili barabara ianze kujengwa.