Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chaumma chaeleza hatua ya kwanza ya utekelezaji kazi

Muktasari:

  • Leo chama hicho kimeendelea na mikutano yake ya Operesheni ya C4C iliyozinduliwa jana katika Viwanja vya Furahisha, jijini Mwanza.

Mara. Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), kimesema  katika kutekeleza sera yake ya Ubwabwa, kikishinda dola katika uchaguzi mkuu wa baadaye mwaka huu, shughuli yake ya kwanza ni kwenda kuondoa ushuru kandamizi kwenye bidhaa za chakula.

Kimesema kwa hali ilivyo sasa, bidhaa nyingi za chakula yakiwamo mafuta, sukari zinatozwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) wa asilimia 18, wakati Watanzania wengi hawana uwezo wa kuilipa.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano Juni 4, 2025 na Kaimu Makamu Mwenyekiti wa chama hicho- Bara, Devotha Minja alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Kata ya Nyamatare, Kijiji cha Kamegesi mkoani Mara, ikiwa ni  muendelezo wa mikutano ya Operesheni yao ya C4C iliyozinduliwa jana katika Viwanja vya Furahisha, Mwanza.

"Tunadhamira ya kweli ya kwenda kushindana na CCM katika uchaguzi mkuu mtuelewe, tukishinda dola, katika kutekeleza sera yetu ya Ubwabwa, tunaenda kuondoa ushuru unaotozwa kwenye bidhaa za chakula kama sukari, mchele, mafuta na bidhaa zingine ili kuleta unafuu wa maisha,” amesema Minja.

Amesema Watanzania wengi wanapitia maisha magumu yanayopanda kila uchwao licha kutimiza miaka 60 tangu nchi ipate uhuru, lakini  wanaofaidi ni kundi la watu wachache.

"Kila tunakopita hakuna Mtanzania mwenye uso wa furaha, CCM imetufikisha hapa, wanawake hata wakipaka vipodozi  uso haubadiliki.

"Wafanyabiashara, wakulima na wafugaji, hali ni ngumu, Chaumma tunakataa tukiingia madarakani ni kwenda kupambana na hawa jamaa ili kuondoa vilio vya wananchi kwa kwenda kutoa ushuru kandamizi," amesema Minja.

Kiongozi huyo amesema kwa sasa wanahitaji wawakilishi wengi bungeni na madiwani na wameona wakisusia uchaguzi haiwezi kuwa njia sahihi ya kuwasaidia wananchi kuondokana na shida wanazopitia.

"Tumesema jukumu letu ni kwenda kupambana na CCM ili wananchi wetu wapate furaha na nuru, jambo hili litafanikiwa ikiwa wote mtakuwa mstari wa mbele kukiunga Chaumma na kuwapatia kura wagombea wao," amesema Minja.

kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chaumma, Hashimu Rungwe amesema licha ya chama hicho kuwa na dhamira ya kweli ya kwenda kubadilisha maisha ya watanzania kupitia sera zake, lazima kiungwe mkono.

"Tunahitaji mtuunge mkono ili tuende tukaigaragaze CCM, ili wasiendelee kutuletea mambo zao, tunaenda kupambana nao hatuwezi kususia mapambano, tuwaache pembeni wanaotaka kususia," amesema Minja.

Amesema kwa kuwa CCM imeshikilia ufunguo wa uchaguzi wangesema hautafanyika,  wangeamini kwa kuwa wananchi wanaenda kufanya uamuzi Oktoba, wamedhamiria kuingia kwenye mapambano.

"Kukataa uchaguzi tutakuwa tumejiunguza wenyewe na sisi tumesema lazima tuingie uwanjani kwenye mapambano, tumewapokea hawa wenzetu ili tukashiriki mapambano," amesema Rungwe.

Amewataka wananchi kupuuza maneno yanayosemwa na baadhi ya watu kuwa chama hicho kimenunuliwa.

"Msimamo wetu hatukubaliani na CCM washinde bila kupingwa uchaguzi ujao na kutufanya tukateseke tena miaka mitano ijayo tutakuwa tumejikaanga wenyewe," amesema nakuongeza;

"Chaumma hatununuliki na hata wakija hawawezi kufika bei, hao ni wazushi tu hawana hoja, mnapaswa kuwapuuza," amesema Rungwe.

Katika hatua nyingine, Catherine Ruge amewashukuru wananchi hao kwa  mapokezi mazuri na kumpatia fimbo ili awe kiongozi wao daima, huku akisema yeye yuko tayari kuongoza jamii hiyo katika mazingira yoyote.

"Siku zote nimekuwa sauti yenu kusemea changamoto mnazopitia na siwezi kukaa kimya, nitaendelee kupigania haki zenu kwa kuwa mmenilea kwa wivu mkubwa na kunisomesha kwa ng'ombe mliofuga kwa shida,” amesema Ruge.

Amekiri kuhama chama na kujiunga na chama kipya cha Chaumma, lakini hajasaliti mapambano, amekihama chama kile alichokuwepo kwa sababu kimerudi nyuma na kukosa uelekeo wa kupigania haki za wananchi.

"Siwezi kukaa Dar es Salaam kimya wakati  wananchi wa Jimbo la Serengeti wanapata shida, ninao huo wajibu wa kulipa fadhila nyingi mlizonifanyia kwa kuja kuwaongoza katika njia sahihi ili mnufaike,” amesema Ruge.

Amesema anakiri kuwa Serengeti wana muwakilishi bungeni, lakini tangu amepata fursa hiyo, hajawahi kwenda kwa wananchi hao kusikiliza kero zao, hivyo ameona udhaifu huo na anaufanyia kazi mwaka huu.