Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chadema yatoa pole ajali iliyouwa 28, majina yawekwa wazi

Muktasari:

  • Chadema imetoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu zao katika ajali iliyoua 28 mkoani Mbeya, huku ikiwapongeza wahudumu wa afya wanaoendelea kutoa huduma kwa majeruhi.

Dar/Mbeya. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeungana na wadau wengine kutoa salamu za pole kwa familia zilizopoteza ndugu na jamaa katika ajali ya gari mkoani Mbeya.

Ajali hiyo, imetokea usiku wa Jumamosi Juni 7, 2025 katika eneo la Mlima Iwambi, mkoani Mbeya na kusababisha vifo vya watu 28 huku wengine wanane wakijeruhiwa.

Ajali hiyo, ilihusisha lori aina ya Scania lililokuwa limebeba shehena ya unga kutoka Dar es Salaam kuelekea Zambia, lililogonga kwa nyuma magari mawili ya abiria aina ya Mitsubishi Rosa na Toyota Lite Ace na hatimaye kuanguka katika bonde la Mto Mbalizi.

Chanzo cha ajali kinasadikiwa ni uzembe wa dereva wa lori kushindwa kulimudu gari kwenye mteremko. Dereva huyo wa lori alivunjika miguu yote na yupo chini ya ulinzi wakati akiendelea na matibabu.

Taarifa ya Chadema iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi, Brenda Rupia, iliyotolewa jana Jumapili Juni 8, 2025 imeeleza kusikitishwa na ajali hiyo.

"Tunatambua majonzi, huzuni na mshtuko mkubwa mlionao katika kipindi hiki kigumu. Tunawaombea faraja, subira na nguvu kutoka kwa Mwenyezi Mungu ili muweze kuvumilia machungu ya msiba huu mkubwa," imeeleza.

Imeeleza Chadema inaungana na wote kwa moyo wa maombolezo na kuwapa pole kwa msiba huo uliotikisa Taifa.

Aidha, chama hicho, kimewatakia majeruhi wote uponaji wa haraka na kuimraika afya zao.

"Tunapongeza jitihada za wahudumu wa afya, pamoja na wadau wote waliosaidia katika kutoa huduma za haraka kwa waathirika wa ajali hiyo," imesema taarifa hiyo.

Katika hatua nyingine, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga alisema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori, Philip Mwashibanda kushindwa kulimudu katika mteremko huo.

Kuzaga alisema dereva anashikiliwa na polisi akiwa hospitali akiendelea na matibabu na majeruhi wengine wanaoendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali Teule ya Ifisi.

"Waliofariki ni 28, wanawake 14, wanaume 14 na majeruhi tisa, mmoja alifariki dunia na kubaki wanane, baadhi yao ni dereva wa lori aliyevunjika miguu yote na Baraka Samuel ambaye ni dereva wa gari la abiria," alisema Kuzaga.

Kuzaga alisema lori hilo lililokuwa na tela lake lilikuwa limebeba shehena ya unga likitoka Dar es Salaam kwenda nchini Zambia.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Ifisi, Dk Morice Martin alisema kati ya watu 28 waliofariki dunia, mmoja pekee ndiyo alifariki wakati anaendelea na matibabu na wengine wote walifikishwa wakiwa wamefariki.

Dk Martin alisema miili 25 kati ya 28 imetambuliwa.


Waliofariki hawa hapa

Baadhi ya majina waliofariki dunia ni, Furaha Gabriel, Josephine Hagai, Joseph Hagai, Odfen Simon, Lydia Gambi, Aman Daud, Mecia Zabron, Edna Mwangomita na Derick Ndanya wote wakazi wa Mbalizi mkoani Mbeya.

Wengine waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni Elisiana Mwsifu, Narice Mwasifu wakazi wa Mbabu na Juma Ramadhan, Deborah Wilson, Gwekelo Zakaria na Lawrence Semwanza wakazi wa Mbalizi.