Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watu 28 wafariki ajalini Mbeya, saba wajeruhiwa

Muktasari:

  • Ajali hiyo imetokea jana saa 1:30 usiku ikihusisha magari matatu katika barabara kuu ya Tanzam, ambapo Lori hilo lilikuwa na shehena ya unga ikitokea Dar es Salaam kwenda Tunduma mkoani Songwe kuyagonga magari mawili  na kusababisha vifo vya watu 28.

Mbeya. Watu 28 wamefariki dunia na wengine wanane kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matatu ikiwamo lori katika mlima Iwambi jijini Mbeya.

Akithibitisha ajali hiyo, Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema ajali hiyo imetokea jana Jumamosi, Juni 7, ambapo watu 27walifariki papo hapo na majeruhi kuwahishwa Hospitali teule Ifisi iliyopo Mbalizi.

Amesema katika barabara kuu ya Tanzam, kutokea Mbeya kwenda Tunduma, gari aina ya lori likiwa na tela likiendeshwa na dereva Philip Mwashibanda (33) liligonga magari mengine mawili.


Amesema katika magari hayo yaliyokuwa na abiria yaligongwa na lori hilo, kisha kutumbukia kwenye korongo ulipo Mto Mbalizi na kusababisha vifo na majeruhi hao.

"Baada ya kugonga magari hayo yalitumbukia korongoni na kukita kwenye gema na kingo za mto, jana hiyo walifariki watu 27 na leo asubuhi tumepata taarifa ya majeruhi mmoja kufariki na kufikia idadi hiyo" amesema Kamanda Kuzaga.

Endelea kufuatilia zaidi mitandao ya Mwananchi