Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Abiria afariki dunia ajali ya bodaboda, basi

Baadhi ya mashuhuda waliokuwepo katika eneo la tukio la ajali lililotokea katika barabara kuu ya kwenda Mwanza katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga.

Muktasari:

  • Kamanda amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo imesababisha kifo cha mtu mmoja mkazi wa Kata ya Ngokolo anajulikana kwa jina la Amani Hamis (26) aliyekuwa abiria wa pikipiki.

Shinyanga. Mtu mmoja amefariki dunia kutokana na ajali iliyohusisha basi la abiria na pikipiki.

Aliyefariki kwenye ajali hiyo ni Amani Hamis, aliyekuwa abiria kwenye pikipiki hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na Emmanuel Frednand.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akieleza kwamba wamemebaini chanzo cha ajali hiyo kuwa ni uzembe wa dereva wa basi la abiria.

Akizungumza na Mwananchi leo Juni 7, 2025 kuhusiana na ajali hiyo, Magomi amesema ajali hiyo imetokea eneo la mataa ya barabara kuu ya kwenda Mwanza, iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga.

“Ajali hiyo imetokea leo Juni 7, 2025 ambapo basi la abiria linalomilikiwa na kampuni ya Capricon, liligonga pikipiki iliyokuwa ikiendeshwa na Emmanuel Frednand, na kusababisha kifo cha abiria wa pikipiki, Amani Hamis (26),” amesema Magomi.

Pia, ameeleza: “Dereva wa pikipiki ambaye ni majeruhi amepelekwa hospitali kwa matibabu kwa sababu amevunjika mguu, mwili wa marehemu umehifadiwa katika chumba cha maiti na baadaye utakabidhiwa kwa familia kwa ajili ya shughuli za mazishi, lakini pia dereva wa basi alitoroka baada ya ajali hiyo naye pia bado anatafutwa na jeshi la polisi.”

Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ajali iliyotokea ni kama kutoelewana kati ya dereva wa pikipiki na dereva wa basi, ndipo chanzo cha ajali kutokea.

“Dereva wa basi aliwasha ‘double indicator’, nahisi dereva pikipiki alidhani basi linanyooka na barabara, kumbe linakata kona na pikipiki ikakata kona, ndipo ajali ilipotokea marehemu amegongwa kichwani,” amesema Paulo John.

“Basi lilikuwa linakata kona na pikipiki inakata kona ndipo walipogongana pikipiki ilikuwa imebeba abiria mmoja ambaye ndiye amefariki dereva pikipiki yeye aliruka pembeni,” amesema Shida Shadrack.