Chadema hapajapoa, Lissu atengua uteuzi wa Catherine Ruge

Muktasari:
- Ndani ya siku tatu wajumbe wawili wa sekretarieti ya Chadema uteuzi wao umetenguliwa kwa nyakati tofauti na mamlaka tofauti za uteuzi wao.
Dar es Salaam. Chadema bado hapajapoa ndivyo unavyoweza kueleza. Hii ni baada ya Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu kutengua uteuzi wa Catherine Ruge aliyekuwa Mjumbe wa Sekretarieti na Mtaalamu wa Dawati la Jinsia.
Ndani ya siku tatu wajumbe wawili wa sekretarieti uteuzi wao umetenguliwa kwa nyakati tofauti na mamlaka tofauti za uteuzi wao.
Aprili 2,2025 Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika alitengua uteuzi wa Julius Mwita aliyekuwa Katibu wa Sekretarieti ya Kamati Kuu ya Chadema, akidaiwa kwenda kinyume na msimamo wa chama hicho wa No Reforms, No Election (Bila mageuzi, hakuna uchaguzi), lakini mwenyewe amedai kuondolewa kwake ni chuki na visasi vya uchaguzi.
Ruge ambaye ni Katibu Mkuu wa zamani wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), uteuzi wake umetenguliwa leo Jumamosi Aprili 5, 2025 na Lissu aliyepo katika ziara ya chama hicho mikoa ya Kusini akinadi ajenda ya No Reforms, No Election.
Mwananchi limemtafuta Ruge ambaye amesema,“ Ni kweli nimetenguliwa, lakini sijaambiwa sababu labda uulize mamlaka za uteuzi wao ndio watakuwa na sababu,” amesema Ruge.
Alipoulizwa kama amepewa barua ya uamuzi huo, Ruge amesema, “nilishapewa barua ya kutenguliwa nafasi hii muda kidogo umepita,” amesema Ruge ambaye ni mbunge wa zamani wa viti maalumu Mkoa wa Mara.
Kupitia akaunti yake ya X, Mkurugenzi wa mawasiliano na uenezi wa Chadema, Brenda Rupia ameandika,” Mwenyekiti wa chama (Tundu Lissu) leo Aprili 5, 2025 ametengua uteuzi wa mjumbe wa sekretarieti na mtaalamu wa dawati la jinsia @catherineruge.
“Operesheni No Reforsm, No Election inaendelea kuchanja mbuga kanda ya kusini.