Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CCM yavuna Sh3.5 bilioni za fomu ubunge, udiwani

Muktasari:

  • Leo Alhamisi, Julai 3, 2025 katika ofisi ndogo za CCM jijini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafuzo wa chama hicho, Amos Makalla amekutana na waandishi wa habari na kuelezea kinachoendelea ikiwemo ratiba za mchujo.

Dar es Salaam. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimejikusanyia zaidi ya Sh3.5 bilioni kutoka kwa watia nia wa udiwani, wabunge na uwakilishi katika kinyany’anyiro cha kupata fursa za kukiwakilisha kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Leo Alhamisi, Julai 3, 2025 katika ofisi ndogo za CCM jijini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafuzo wa chama hicho, Amos Makalla amekutana na waandishi wa habari na kuelezea kinachoendelea ikiwemo ratiba za mchujo.

Makalla amesema makundi mbalimbali ikiwemo vijana, wanawake na wasanii wamejitokeza na hiyo inaonyesha CCM ina hazina kubwa lazima ilindwe kwa kutenda haki katika mchakato huo.

"Takwimu za haraka waliochukua fomu kwa majimbo Tanzania Bara wako 3,585 na Zanzibar katika majimbo wako 524, jumla katika majimbo tu wanachama walionyesha nia wako 4,109 na tuna majimbo 272 unaweza kuona ni namna gani hamasa ilivyokuwa kubwa," amesema Makalla.

Amesema upande wa uwakilishi Zanzibar waliochukua fomu za kutia nia wako wanachama 503 wakati Umoja wa Wanawake (UWT) wako 623 Tanzania Bara na ndani yake wako 61 wa makundi maalumu lakini Zanzibar wamechukua wanane.

"Viti Maalumu uwakilishi kule Zanzibar wako tisa kwa hiyo jumla ya UWT waliojitokeza wako 640 lakini umoja wa vijana wamechukua 161 na Zanzibar wako saba lakini Jumuiya ya Wazazi wako Tanzania Bara 55 na Zanzibar pamoja na uwakilishi jumla wapo 575," amesema. 

Makalla amesema katika ubunge na uwakilishi jumla ni 5,475. Kwa kuwa fomu za ubunge zilikuwa zinatolewa kwa Sh500,000, hii ina maanisha kwa idadi ya waliochukua 5,475 chama hicho tawala kimejikusanyia zaidi ya Sh2.7 bilioni.

Amesema upande wa ngazi ya udiwani kuna takribani kata 3,960 bado haijafanya majumuisho na wanatarajia kuwa na watia nia zaidi ya 15,000 nchi nzima katika nafasi hiyo, inayojumuisha madiwani na wale wa viti maalumu.

Gharama za fomu za udiwani ni Sh50,000. Hii ina maanisha kama ni 15,000 watakuwa wamejitosa basi itakuwa imejikusanywa Sh750 miloni.