Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ADC yajipa moyo uchaguzi kuwa huru na wa haki

Katibu Mkuu wa ADC, Hassan Doyo katika moja ya mkutano na waandishi wa habari. Picha na Maktaba

Muktasari:

  • Katibu Mkuu wa ADC, Hassan Doyo, amesema uamuzi wa Mahakama Kuu uliotengua utaratibu wa wagombea kupita bila kupingwa umeleta matumaini ya kuwa na uchaguziu ulio huru na wa haki siku za usoni.

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa ADC, Hassan Doyo, amesema uamuzi wa Mahakama Kuu uliotengua utaratibu wa wagombea kupita bila kupingwa umeleta matumaini ya kuwa na uchaguziu ulio huru na wa haki siku za usoni.

Doyo ameyasema hayo leo Jumatano Machi 5, 2023 alipokuwa akichangia mada katika mjadala wa Twitter Space, unaoendeshwa na Mwananchi Communications Ltd uliobeba mada “Zuio la wabunge kupita bila kupingwa litachagiza uwezo wa uchaguzi huru 2025?”

Doyo ameseama wanaopenda mambo ya kupita bila kupingwa wamekuwa wakifanya mbinu za kuruhusu mazingira yao na sasa sheria inakwenda kuweka wazi kwamba hakuna kupita bila kupingwa.

Mchangia mada mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Innocent Temu, amesema kwa hatua iliyofikia na mahakama nchi inaelekea kwenye jambo zuri, kwani hata kungekuwa na Tume Huru kama hili la kupita bila kupingwa lingekuwa bado lipo isingesaidia.

Aidha ameipongeza Mahakama wa hatua hiyo na kuongeza kuwa ukiongezea na madai ya Tume huru, kunakoelekea watu itabidi kushindana kwa hoja kweli.