Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Mwanasheria Mkuu wa Serikali asimamie masilahi ya wananchi’

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Eliezer Feleshi.

Muktasari:

  • Mwanasheria Jebra Kambole ameitaka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kusimamia masilahi ya wananchi kuliko mihimili mingine ya Dola.

Dar es Salaam. Wakili na Mwanasheria maarufu, Jebra Kambole amesema, ifike mahali Mwanasheria Mkuu wa Serikali awe anasimama na wananchi badala ya Bunge.

Sambamba na hilo amemtaka awe wa kwanza kupinga sheria mbovu ambazo zimekubwa zikipitishwa na chombo hicho kwa kuwa hata suala la mgombea binafsi halina maslahi kwake.

Msimamo wa Kambole umekuja kufuatia kauli ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Eliezer Felesh aliyeulizwa na Mwananchi kuhusu hukumu ya Mahakama Kuu iliyotengua utaratibu wa wagombea kupita bila kupingwa wiki iliyopita, ambapo alisema uamuzi huo hauna muda mrefu na kwamba unahitaji utafiti kwanza.

Akichangia mada katika mjadala wa Twitter Space, unaoendeshwa na Mwananchi Communications Ltd uliobeba mada “Zuio la wabunge kupita bila kupingwa litachagiza uwezo wa uchaguzi huru 2025?” leo Jumatano Machi 5, Kambole amesema,

“Mwanasheria Mkuu wa Serikali anapaswa kuheshimu uamuzi wa mahakama na kuzingatia haki za binadamu kwenye utendaji wake, kwani kwa sasa Mwanasheria mkuu anajikuta ana kazi nyingi , yeye anasimamia Bunge, Serikali na Mahakama kitu ambacho sio sahihi,” amesema.

Hata hivyo, mwanasheria huyo amesema hakuna faida ambayo Mwanasheria Mkuu anapata kwa watu kupita bila kupingwa hivyo haoni sababu ya kutetea au kulinyamazia jambo hilo.

Kwa upande wake mwanaharakati, Tito Magoti, ameitaka Serikali kutekeleza hukumu hiyo.