Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ACT Wazalendo: Kukosa nguvu ya kuamua kiongozi ni utumwa


Muktasari:

  • Chama cha ACT Wazalendo kimeendelea na operesheni ya majimaji mkoani Kigoma, huku kikitaka wananchi wasipokwe haki ya kupiga kura.

Kasulu. Chama cha ACT Wazalendo kimesema thamani ya raia ipo kwenye nguvu ya kuamua nani awe kiongozi wake, ikitokea amepokwa haki hiyo anabaki kuwa mtumwa ndani ya Taifa lake.

Kwa mujibu wa chama hicho, hatua ya raia kupokwa haki hiyo kunasababisha waongozwe na viongozi wasiowataka, hali inayosababisha wengi wakose ari ya kushiriki michakato ya uchaguzi.

Hayo yameelezwa leo Jumatano Julai 2, 2025 na Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Bara, Issihaka Mchinjita alipozungumza mbele ya wananchi wa Kijiji cha Rungwe Mpya, ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya operesheni majimaji.

Amesema hatua ya wananchi kupokwa haki na nguvu ya kura yao, imesababisha wengi wapoteze ari ya kushiriki uchaguzi, kiasi cha wengine kuona hakuna haja ya kwenda kupiga kura.

Ingawa zipo sababu za msingi za wananchi kupoteza ari hiyo, amesema historia inaonyesha hakuna mafanikio yaliyopatikana kwa kupoteza mwamko wa kushiriki uchaguzi.

Mchinjita amesema chama chake kinatambua changamoto za kisheria na haki ndani ya mchakato wa uchaguzi, lakini hawaoni sababu ya kutoshiriki kwa kuwa kufanya hivyo, kunawafaidisha watawala.

"Watu wameanza kujadili katika nchi hii kwamba bora tuwaachie CCM wenyewe, kwa sababu uchaguzi umepoteza thamani na kura ya raia imepoteza nguvu yake," amesema.

Mitazamo waliyonayo wananchi kuhusu uchaguzi, amesema ndiyo iliyokifanya chama hicho kione sababu ya kuja na operesheni majimaji itakayohusika na kuwahamasisha wananchi baada ya kupiga kura wazilinde.

Amesema lazima kurejea historia ya nchi ya kuunganisha nguvu za raia kukabiliana na udhalimu uliokuwa unafanyika.

Amesema uamuzi wa kuiita operesheni majimaji ni kurejea harakati za wazee waliojitoa kupambana na Serikali ya kikoloni katika mazingira magumu kwenye vita ya Majimaji.

Amesema mapambano hayo, yalitokana na ukweli kwamba Serikali ya kikoloni haikuwa imepewa ridhaa ya wananchi, badala yake ilijiweka yenyewe madarakani.

Hoja ya Mchinjita iliungwa mkono na Kiongozi wa chama hicho, Dorothy Semu aliyesema ili kutoka katika mazingira magumu ya michakato ya uchaguzi, lazima raia wahamasishane na kuelewana kuwa wana nguvu ya kuamua nani awe kiongozi na sio kuwekewa.

"Pale ambapo wapinzani walisusia watawala, walichukua nafasi zote na kutengeneza sheria kandamizi zaidi ili kuendelea kuwa wababe na nguvu zaidi, kama ilivyotokea katika uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2019.

"Watawala watafurahi sana kuona kuwa hatushiriki uchaguzi, sisi hatutawapa hiyo nafasi, tutashiriki na mshindi anayetokana na kura nyingi za wananchi lazima atangazwe," amesema.

Amesema chama hicho kinashiriki uchaguzi kwa sababu mchakato huo sio mali ya chama cha siasa, bali ni wananchi wote wanatumia haki yao kupiga kura.