Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jenerali Sani Abacha: Dikteta aliyeacha makovu mengi Nigeria

Muktasari:

Abacha mzaliwa wa Kabila la Borno kutoka Kanuri, sehemu kubwa ya maisha alikulia katika Mji wa Kano, Nigeria. Alisoma mafunzo ya kijeshi kwenye Chuo cha Jeshi cha Nigeria.

Jenerali Sani Abacha alikuwa Rais wa 10 wa Nigeria kuanzia mwaka 1993-1998. Abacha aliyezaliwa Septemba 20, 1943, alifariki dunia katika mazingira ya kutatanisha yaliyoacha maswali mengi kuliko majibu.

Mbali na kifo chake cha utata cha Juni 8, 1998, lakini pia staili ya utawala wake imeacha majeraha na maumivu makubwa pengine kuliko watawala wengine wote wa nchi hiyo.

Abacha aliongoza nchi kidikteta kama vile mali ya familia na kutokana na hali hiyo, mara kwa mara alijikuta akinyoshewa vidole na jumuiya mbalimbali za kimataifa.

Lakini pia kutochukua juhudi zozote za kukomesha vitendo vya rushwa, huku naye akitajwa kama kiongozi mla rushwa kupindukia, kulimfanya kuchukiwa zaidi ndani na nje ya Nigeria.

Kumbukumbu nzuri pekee ya utawala wake ni kufanikiwa kupunguza mzigo wa madeni ya nje kutoka Dola za Kimarekani 36 bilioni 1993 kufikia dola 27 bilioni 1997.

Aliongeza pato la nchi kupitia fedha za kigeni kutoka Dola 494 milioni mwaka 1993 hadi Dola 9.6 bilioni 1997. Alipunguza mfumuko wa bei kutoka asilimia 54 enzi za Ibrahim Babangida hadi asilimia 8.5 kati ya 1993 na 1998.

Pamoja na rushwa na ukiukwaji wa haki za binadamu, Abacha anatajwa kama kiongozi pekee katika historia ya Nigeria aliyefanikiwa kuleta mageuzi ya kiuchumi.

Abacha mzaliwa wa Kabila la Borno kutoka Kanuri, sehemu kubwa ya maisha alikulia katika Mji wa Kano, Nigeria. Alisoma mafunzo ya kijeshi kwenye Chuo cha Jeshi cha Nigeria.

Mwaka 1963, alikwenda kusoma Chuo cha Mons Defence Officers Aldershot, England na baadaye aliporudi Nigeria alijiunga na Chuo cha Jeshi cha Kaduna.

Abacha aliongoza mapinduzi yaliyomuingiza madarakani Jenerali Muhammadu Buhari, kabla ya kumpindua tena mwaka 1983. Novemba 17, 1993, aliipindua Serikali ya muda ya Ernest Shonekan.

 

Lawama:

Utawala wa Abacha ulishutumiwa kwa kukiuka haki za binadamu, huku mwenyewe akipuuza kila aina ya upinzani dhidi yake.

Uamuzi wake wa kumnyonga mwanaharakati Ken Saro-Wiwa ulishutumiwa vikali ndani na nje ya nchi. Pia alipuuzia mbali ombi la kutowafunga Moshood Abiola na Olusegun Obasanjo.

Abacha anadaiwa kujilimbikizia mali nyingi ikiwa ni pamoja na kutorosha pesa na kuziweka kwenye akaunti yake binafsi nje ya nchi akishierikina na kijana wake.

Kifo:

Alifariki dunia Juni, 1998 katika Ikulu ya Villa, Mjini Abuja na kuzikiwa siku hiyo hiyo.

Kifo chake kilizua utata, huku wengine wakisema aliuawa baada ya kuwekewa sumu na makahaba.

Awali, iliilezwa Abacha alionekana akiwa na wanawake wawili wenye asili ya India kutoka Dubai, lakini taarifa ya serikali zilipinga madai hayo na kueleza kifo chake kilitokana na shinikizo la damu.

Baada ya kifo cha Abacha, Jenerali Abdulsalami Abubakar, alishika madaraka kabla ya kurejesha utawala wa kiraia chini ya Rais Olusegun Obasanjo.