Vikoba vimewainua wanawake wengi nchini

Muktasari:
Scolastica Kevela ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Vicoba Tanzania, yeye ni mongoni mwa wadau wakuu wanaoimarisha ustawi wa vikundi nchini , amefanikiwa kushika wadhifa huo kutokana na juhudi alizozionyesha katika kujitolea kuhamasisha wananchi kujiunga ili waweze kujikopesha kwa masharti nafuu, hatua ambayo inawasaidia kujiimarisha kiuchumi.
Uwepo wa vikundi vya Vicoba nchini inaaelezwa kwamba vimesaidia kwa kiasi kikubwa na kuwezesha watu wengi hasa wale kipato cha chini na kile cha kati kujiinua kiuchumi na hivyo kumudu kuendesha maisha katika hali ya unafuu.
Scolastica Kevela ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Vicoba Tanzania, yeye ni mongoni mwa wadau wakuu wanaoimarisha ustawi wa vikundi nchini , amefanikiwa kushika wadhifa huo kutokana na juhudi alizozionyesha katika kujitolea kuhamasisha wananchi kujiunga ili waweze kujikopesha kwa masharti nafuu, hatua ambayo inawasaidia kujiimarisha kiuchumi.
Elimu yake ya juu aliyonayo sasa Scolastica ni Shahada ya Uzamili ya Utawala kutoka Chuo Kikuu Huria anazungumza na gazeti hili akieleza alishawishiwa na hali ya ugumu wa maisha ulisababishwa na kipato kisicho na uhakika miongoni mwa wananchi hasa wanawake ilisababisha kunyimwa frusa za kukopa kwenye taasisi za fedha hasa benki kutokana na kutokuwa na mali za kuweka dhamana ya mikopo ndiyo.
“ Hii hali ndiyo ni sababu mojawapo iliyonishawishi nijione nina jukumu la kushiriki katika kuwawezesha wanyonge wa aina hiyo kuunganisha nguvu ya pamoja kwa kile kidogo walionacho na kukitumia hicho kwa nidhamu ya masharti nafuu ili kujikomboa kiuchumi,” anasema.
Anasema tangu kuanzishwa kwa Vicoba mwaka 2002, vimesaidia watu wengi lakini zaidi wanawake ambao ndiyo wamekuwa na mwitikio wa kujiunga, ambapo kupitia vikundi hivyo wamepata mwamko na wa kushiriki katika kuinua uchumi wa familia, pia wameweza kumiliki uchumi tofauti na ilivyokuwa awali.
“ Vicoba vimekuwa mitaji mizuri ya kuwawezesha wengi kufanya biashara katika hali ya kujiamini, wengine walikuwa wakifanya bishaashara ndogo ndogo kama vile maandazi, vitumbua wameziboresha biashara hizo na kuzifanye ziwe kuwa ikiwamo kumiliki migahawa ya kisasa hivyo kuwavutia wateja,” anasema.
Scolastica pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Uwakala wa Dalali wa Mahakama ya Yono Auction Mart, ambayo wanaimiliki na mumewe Yono Kevela, ametunukiwa Shahada ya pili ya Utawala na Biashara (MBA) kutoka Chuo Kikuu Huria nchini, Shahada ya kwanza ya kimataifa ya mawasiliano ya kompyuta, aliyosomea kwenye Chuo kikuu cha London Metropolitan Tawi la Tanzania.
Akieleza mchango wake katika kuwainua vikundi hivyo anaeleza kuwa amekuwa akitumia muda mwingi kuhamasisha jamii hasa wanawake kujiunga kwenye vikundi na kuanzisha Vicoba ili kuweza kujikwamua kiuchumi.
Anasema amekuwa akihamasisha kupitia mikutano au kwenda moja kwa moja kwenyemasoko ambapo hukutana na makundi maalumu yanayowakutanisha watu wa makundi mbalimbali wakiwamo wenye ulemavu, kwenye, mama lishe waliopo katika maeneo mbalimbali nchini.
“Elimu ambayo tumekuwa tukiwapa wana Vicoba ni pamoja na kutambua jinsi ya kuziboresha biashara walizonazo na kuziboresha au kubuni nyingine mpya, pamoja na kutothubutu kutumia fedha za mikopo kwa mambo yaliyo nje ya miradi yao ili kuepusha kunyang’anywa mali na wanakikundi wenzao baada ya kushindwa kurejesha mkopo,” anasema.
“ Ingawa pia nina majukumu kwenye familia yangu ya watoto wanne nashukuru kuna wengine wanasoma shule za bweni, lakini ninajitahidi kama mama, najua watoto wananihitaji, pia mume wangu natakiwa kumhudumia kwa hiyo nijipamgia muda wa kufanya kazi za kijamii na zile nyumbani,” anasisitiza.
Anasema familia inapokuwa na kipato vikubwa inasaidia katika kuboresha uwezo wao kupitia, afya bora kutokana na lishe na malazi, pia watoto wa familia wanapata nafasi ya kupewa elimu bora kwa kuwa wazazi wanamudu kulipa ada.
Scolastica anasema mafanikio yanayoendelea kujitokeza kwenye Vicoba yanachochewa pia na ushirikiano mzuri walionao na Jimbo la South Caroline kupitia Chuo cha Benedict kwenye mji wa Colombia, Marekani na wamewahi kupata mwaliko wa kwenda kujifunza jinsi vikundi kama hivyo vinavyoendeshwa.
Anafafanua kuwa
Aidan Kumbuku ni Mshauri wa Vicoba katika Makao Makuu ya Vikoba Kijitonyama, anakiri Scolastica ana wito wa kukuza vikundi hivyo, kwani licha ya kushirikiana na viongozi wenzake katika kuvifanikisha, pia amekuwa na juhudi zake binafsi ambazo amekuwa akizifanya ikiwamo kuhamasisha uanzishwaji wa vikundi hivyo ikiwamo katika Jimbo la Segerea .
“ Mfano katika la kipawa amenishirikisha kutoa elimu iliyowezesha kupatikana kwa walimu 30 ambao nao walisaidia kutoa elimu vikaanzishwa jumla vikundi 132 , ambavyo vimefanikiwa kuwekeza milioni 100 na vilizinduliwa rasmi mwezi Machi mwaka huu.
“ Ametusaidia wengi kupita hatua, mfano binafsi katika kikundi chetu sasa ninaweza kukopeshwa hadi shilingi milioni 3, pia nimeweza kuboresha huduma yangu ya kuuza maji kwa ndoo kutoka kwenye matanki nilianza na la lita 3,000 lakini sasa nimenunua la lita 7,000 ikiwa ni pamoja na kuongeza vituo vya mauzo,” anasema Jeni Lambati akitoa ushuhuda.