Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hii ndio familia ya Uhuru Kenyatta

Familia ya Uhuru Kenyatta.

Muktasari:

Sasa ikulu inakaliwa na familia mpya baada ya muda wa urais wa Kibaki kumalizika mapema wiki hii.Familia mpya iliyoingia ni ya Uhuru Kenyatta ambayo ni ya watu watano ambao ni Kenyatta mwenyewe, mkewe Magaret Gakuo na watoto wake watatu; Ngina, Jomo na Jaba.

Siku tano zilizopita nchi ya Kenya ilipata familia mpya ya kwanza (First Family), baada ya ile ya Mwai Kibaki kuondoka katika  ikulu ya nchi hiyo. Familia ya kibaki ilikuwa ya watu saba akiwemo mkewe Lucy Muthoni , watoto; Judy Wanjiku, Jimmy Kibaki, David Kagai na Tony Githinji.

Sasa ikulu inakaliwa na familia mpya baada ya muda wa urais wa Kibaki kumalizika mapema wiki hii.Familia mpya iliyoingia ni ya Uhuru Kenyatta ambayo ni ya watu watano ambao ni Kenyatta mwenyewe, mkewe Magaret Gakuo na watoto wake watatu; Ngina, Jomo na Jaba.

Mkewe, Margaret ni mara chache sana huonekana katika hadhara, si mzungumzaji na mara moja moja sana huongozana na mumewe katika hafla mbalimbali.

Kama alivyo mumewe, Margaret naye anatokea katika familia iliyowahi kushika nyadhifa kubwa nchini humo, baba yake, Njuguna Gakuo aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli nchini humo .

Alisoma katika shule ya kifahari wakati huo iliyoitwa St Andrew katika mji wa Molo. Alikutana na mumewe mjini Mombasa, kabla ya kuwa wapenzi, wachumba na baadaye wanandoa, wawili hao walikuwa marafiki wakufa na kuzikana.

Ambao walikuwa wakienda sehemu mbali mbali pamoja ikiwemo na kupeana ushauri wa mambo mbali mbali kabla ya kila mmoja kuvutiwa na mwenzake na kuamua kuingia kwenye mahusiano.

Walifunga ndoa katika kanisa la Holy Family Basilica jijini Nairobi, mwaka 1989. Pamoja na kuwa Margaret ameolewa na mtoto wa Rais wa kwanza wa nchi hiyo, inaelezwa kuwa amekuwa akiishi maisha ya kawaida.

Kiasi kwamba hakuwa maarufu kama wake wengine wanaoolewa kwenye familia zinazojiweza kama hii ya baba yake Kenyata.

Hakujihusisha na vikundi vya kina mama au taasisi ambazo zingemfanya sikike sana na vile vile hakuwa akipenda kusikika kwenye vyombo vya habari kwa namna yoyote ile.

Hata ukitazama picha zake unagundua kuwa si mpenda makuu, nywele zake zenye mvi nyingi ameziacha hivyo tofauti na wanawake wengi ambao wangependa kujipamba kutokana na uwezo na wadhifa kama huo.

Mara kadhaa amekuwa akinywa kahawa katika migahawa ya kawaida katika mji wa Nairobi, watu wa karibu yake wanasema ni mwanamke asiye na maneno mengi na mwenye aibu nyingi.

Hata ukiangalia kipindi cha kampeni za mumewe tofauti na wake wengine wa wagombea Margaret,alikuwa kimya hakusikika sana,na hata baada ya mumewe kuapishwa kuwa raisi wan chi hiyo hajasikika kama ambavyo wanawake wengi wanafanya.

Licha ya kuwa ni mwenye kuvutia lakini bado hakuwa na maringo alimsikiliza kila aliye karibu nae ,kwa kuwa hakuwa msemaji ilikuwa ngumu kuwasikiliza wasio karibu nae.

Ni mke wa raisi wa aina yake kwani pamoja na kuwa muda mwingi alikuwa mwenyewe familia inayojimudu hakuwahi kuendeshwa alikuwa akiendesha gari lake mwenye ,kwa kuwa sasa amekuwa mke wa Rais huenda akakubali kuendeshwa.