Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tumia siki kutibu maradhi haya

Muktasari:

Siki ni kimiminika chenye ladha ya ugwadu na hutokana na baadhi ya matunda kama vile zabibu au nazi. Hutumika kwa ajili ya kuchachua baadhi ya vyakula au mboga. Wataalamu wa mambo ya tiba wanaikubali kama tiba mbadala. Ina faida nyingi na inatibu maradhi mengi.

Kuvimba mwili

Chukua siki kikombe kimoja changanya na unga wa Hulba kijiko kikubwa kimoja na Khardali kijiko kikubwa kimoja paka mwili mzima. Au chukua siki ya zabibu kikombe kimoja na habasoda ya unga kijiko kimoja chemsha kisha paka kwenye uvimbe na ule vijiko viwili kutwa mara tatu.

Ugonjwa wa Pumu

Tia kijiko cha Habbat-Sawdaa iliyochemshwa katika maji ya yaliyochemshwa kisha unywe moto.

Kuuma mgongo

Changanya asali nusu lita pamoja na siki kikombe cha kahawa, vijiko viwili Habbat-Sawdaa na iwe kitu cha kwanza kunywa wakati wa asubuhi kabla ya kufungua kinywa.

Maradhi ya ngozi

Ugonjwa wa ngozi ni katika maradhi yanayosumbua sana. Na yote yanaweza kutibika kwa siki.

Maradhi haya ni kama m-mba, upele, chunusi, fangasi, miwasho, malengelenge, mapunye, mapwepwe, kunyonyoka nywele, kunuka miguu, kunuka kwapa na mengineyo.

Tiba yake: Sikui kikombe kimoja, changanya na mafuta ya habasoda nusu kikombe changanya na mafuta ya waridi nusu kikombe na ngano nyekundu kikombe kimoja, kisha upake kutwa mara mbili.

Au chukua siki nusu kikombe changanya na mlutulutu kijiko kimoja na kibiriti upele(Sulphur), na maziwa ya unga vijiko viwili na mafuta ya kitunguu saumu nusu kikombe. Paka kutwa mara mbili.

Vile vile unaweza kuchanganya siki nusu kikombe na sufa vikiko vikubwa viwili vya mezani na asali nusu lita na unywe kijiko vijiko viwili kutwa mara tatu. Ni vyema kuonana na mtaalamu wa tiba mbadala kwa ufafanuzi zaidi wa matumizi haya.