Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtu mwenye dalili ya mvunjiko wa mfupa

Muktasari:

  • Basi kama ikikutokea hali hali kama hiyo, usichanganyikiwe kwanza, jaribu kutambua kama mfupa umevunjika au kutenguka au kama misuli au tishu imeumia aidha kwa kuchanika, kujisokota au kwa njia nyingine.

Umewahi kukutana na mtu aliyeanguka na kuwa na dalili zote za kuvunjika mguu au mkono?

Basi kama ikikutokea hali hali kama hiyo, usichanganyikiwe kwanza, jaribu kutambua kama mfupa umevunjika au kutenguka au kama misuli au tishu imeumia aidha kwa kuchanika, kujisokota au kwa njia nyingine.

Inaweza kuwa vigumu kutofautisha majeraha haya na huduma ya eksrei huenda ikahitajika kujua kwa hakika.

Kama huwezi kujua iwapo mfupa umevunjika, umetenguka au msuli au tishu kuumia, iweke sehemu hiyo ya mwili katika nafasi moja bila kutikiswa huku ukitafuta msaada.

Nasema hivyo kwa sababu hutakiwi kuutikisa mfupa uliovunjika hadi mtu mwenye uzoefu wa kunyoosha mifupa atakapourudisha katika nafasi yake na kuufunga kwenye plasta ngumu au piopii.

Ili kusaidia ubaki sehemu moja bila kutikisika, tengeneza banzi kutoka kwenye kadibodi (karatasi ngumu iliyokunjwa), kipande chepesi cha ubao bapa, au kitu kingine kigumu kilichonyooka.

Namna ya kutoa huduma ya kwanza

Weka mkono au mguu katika nafasi yake ya asili ya kupumzika. Kiwiko kinapaswa kuwa kimepinda kidogo kama ni mkono.

Zungushia bandeji, shashi, kitambaa chepesi au tumia mkono wa shati.

Pumzisha mkono kwenye kibanzi. Weka kitambaa kilichoviringishwa ndani ya kiganja.

Kama jeraha liko kwenye mguu, banzi lifungwe pembeni. Zungushia bandeji au kitambaa kwenye banzi ili libaki kwenye nafasi inayohitajika.

Wapo watakaouliza kwanini unashauriwa kutumia fimbo au mbao ngumu, lengo ni kuzuia mguu au mkono kusogea kwasababu unaweza kusababisha maafa zaidi kwenye mishipa ya damu, mishipa ya fahamu na misuli. Pia hupunguza maumivu na kuvuja kwa damu.

Baada ya mgonjwa kupata huduma hiyo ya kwanza, kinachofuata ni kumpeleka kwenye kituo cha afya kwa matibabu zaidi.

Imeandaliwa na Elizabeth Edward