Mwenyekiti UVCCM aeleza changamoto, mafanikio ya vijana

Muktasari:
Swali: Je, tangu umeingia katika umoja huu ni changamoto gani umekutana nazo?
Jibu: Nafasi yenyewe ni kubwa, Mwenyekiti ni kiongozi mkuu wa Umoja wa Vijana lakini pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya chama kwa msingi huo kama kiongozi wa taasisi kuna shughuli za kisiasa, kiutumishi na kiutawala lakini lipo jukumu kubwa zaidi ambalo CCM kimeikabidhi jumuiya nalo ni kuandaa viongozi. Kwa maana ya kugroom viongozi wa chama na Serikali, hili ni jukumu kubwa ambalo ndiyo hasa msingi wa kuanzishwa kwa jumuiya ya vijana.
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Kheri James juzi amefanya ziara katika ofisi za Gazeti hili na kufanya mahojiano kuhusu mambo mbalimbali yakiwamo hali ya siasa, mikakati yake katika umoja huo na changamoto anazokutana nazo na hii ni sehemu ya mahojiano hayo.
Swali: Je, tangu umeingia katika umoja huu ni changamoto gani umekutana nazo?
Jibu: Nafasi yenyewe ni kubwa, Mwenyekiti ni kiongozi mkuu wa Umoja wa Vijana lakini pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya chama kwa msingi huo kama kiongozi wa taasisi kuna shughuli za kisiasa, kiutumishi na kiutawala lakini lipo jukumu kubwa zaidi ambalo CCM kimeikabidhi jumuiya nalo ni kuandaa viongozi. Kwa maana ya kugroom viongozi wa chama na Serikali, hili ni jukumu kubwa ambalo ndiyo hasa msingi wa kuanzishwa kwa jumuiya ya vijana.
Tunawaandaa vijana ili kuwa viongozi wa chama na Serikali. Na kama mnavyoona asilimia 90 ya vijana wote ambao wanakuwa quality origin yake ni UVCCM. Tunaamini kupitia huku wakitengenezwa vizuri wakafikia viwango vile wanatosheleza kwenda kufanya kazi vizuri.
Lakini, jukumu la pili ni kuifanya taasisi hiyo kujiendesha. Taasisi ina mipango, waajiriwa, miradi na mali kwa hiyo ina involve wataalamu katika ngazi za idara na makatibu wasaidizi wakuu ambao wanafanya kazi za kitaaluma katika kusimamia hizi shughuli za uendeshaji za kila siku.
Hivyo, kwanza ni matarajio ya vijana wenyewe kwa sababu wanajua hii ndiyo taasisi inayowatengeneza kwenda kuwa viongozi. Kila kijana anatamani awe ni miongoni mwa wale ambao kwa muda huu uliopo awe ameaminiwa. Ni changamoto kubwa kwa sababu mawasiliano ya chama na jumuiya huwa yanapitia hapo kwa mwenyekiti wa vijana na wasaidizi wake kwamba ni nani katika sisi ana-qualify kwenda wapi kwa hiyo mahitaji ya vijana wengi kwenda kuhudumia chama na Serikali ni makubwa kwa hiyo ni nani kwa wakati gani aende na wana qualify. UVCCM ina vijana wenye uwezo mkubwa wengi lakini nafasi ni chache.
Pili ni mahitaji ya uendeshaji; kama tunavyofahamu jumuiya ni taasisi ya siasa lakini inajiendesha kupitia miradi yake kupitia vitega uchumi mbalimbali ni ngumu kufanya shughuli za kisiasa na kibiashara, lakini tunashukuru tumeweza kuitatua hiyo changamoto kwa kuwa na wawekezaji ambao hawapo direct na politics kwa hiyo miradi mnaiweka kama miradi na siasa ni siasa, hivyo sasa tunakutana na miradi yenu katika kipindi cha malipo ili kuweza kuendesha shughuli zetu japo changamoto zaidi ni mahitaji ya vijana na matarajio kwa chama na Serikali yao.
Kuna tatizo la ajira, wanaamini UVCCM ndiyo jumuiya yenye sauti, sasa ajira sisi tunapataje ina maana hapo tutafute direction (mwelekeo).
Lakini, pia zipo haki na maslahi ya vijana ambako wanaamini umoja ndiyo wakili wao, sasa wanapo kwama wanaona tunakwamaje na jumuiya ipo na ndiyo maana mwenyekiti wa vijana anakuwa mjumbe wa Kamati Kuu ambayo anaiendesha Rais, wajumbe ni Waziri Mkuu, Spika wa Bunge,
INAENDELEA UK 22
INATOKA UK 21
vyombo vyote vya maamuzi katika nchi hii wakuu wake ni wajumbe wa CC kwa hiyo wanaamini kwa kuwa na mwenyekiti wetu yumo mle ndani maslahi yetu yatatatuliwa na maamuzi yatatolewa.
Lakini wanafunzi wa chuo kikuu wanahitaji kupata mkopo, pia ni kazi yetu unakuta mtu hana wazazi anafika pale anaambiwa huna sifa kwa nini kwa kuwa tu amesoma shule binafsi lakini ni ‘mporipori’ mwenzetu, masikini hali yake ni mbaya inajulikana. changamoto kama hizi ni zetu ukiacha zile zinazoibuka kulingana na misimu na hali ya wakati fulani kwa sababu hii ni taasisi, zipo zinaibuka kutokana na matukio.
Mtazamo wangu ndugu zangu ukiwaona watu wanahitimu kuna kazi kubwa, kuna watu wamesomeshwa kwa mazingira duni wengine wamesomeshwa na paroko katika misheni unamaliza kidato cha sita unataka kwenda chuo kikuu wanasema haiwezekani, kisa amesoma shule binafsi.
Wengine masikini wapo wanaosomeshwa na watu lakini baadaye siyo reliable tena. Au wamesoma kimkopo mkopo tu, tuangalie aliyesoma binafsi amesoma kwa mpango gani vinginevyo tutawapoteza na kuwanyima haki vijana wengi.
Swali: Je, UVCCM mmeshahakiki miradi yenu baada ya Mwenyekiti Taifa Rais John Magufuli kuteua kamati maalumu ya kuhakiki? Na je, miradi hiyo inawasaidia vipi wakati mara nyingi mnashindwa kulipa watumishi mishahara kwa wakati?
Jibu: Kama ambavyo ameagiza mwenyekiti Taifa lakini by the time na sisi tukaunda kamati ndogo kwa sasa tunasubiri akiwasilisha ripoti yake na sisi tutampa ya kwetu.
Kuhusu miradi, si miradi yote inakuwa ina pay kulingana na mahitaji kuna wakati mnakuwa na mahitaji lakini mradi unakuwa hauja mature. Kuna wakati miradi yenu inakuwa nayo lakini mahitaji yenu ya fedha yanakuwa nje ya wakati. Na jambo lingine katika zoezi la uhakiki mnagundua kuwa kuna mengine mnayo lakini by contant siyo mizuri mingine faida siyo nzuri mingine haizalishi lakini ipo katika hesabu lakini haipo katika uzalishaji. Kwa hiyo hizo ndiyo changamoto ambazo tunazo na kwa miezi hii minne tuliyokaa tumeona hivyo tunayo nafasi ya kutaona namna bora ya kutumia hii miradi katika malengo yetu ya baadaye.
Swali: Mwenyekiti Taifa aliwahi kusema hakuchagua vijana kwenye nafasi za uongozi serikalini kwa sababu UVCCM hawakuwaletea majina je, sasa hali ikoje?
Jibu: Utaratibu anapelekewaje na anapelekewa na nani hilo ni suala lingine, lakini mimi tangu mwenyekiti wa chama Taifa achaguliwe tumekuwa na mahusiano yetu kama taasisi ni makubwa sana kwa hiyo vijana wategemee makubwa zaidi. Ilikuwa ni jambo la kiofisi halikuwa jambo la mtu.
Swali: Vipi kuhusu suala la Joketi ukweli ni nini ?
Jibu. Hili ni suala sipendi kulijibu kwa sababu halina tija sana lakini kwa faida ya umma, hii ni taasisi na inafanya maamuzi wakati wowote kulingana na tija na mahitaji kwa hiyo kama ambavyo Mwananchi mnafanya mabadiliko sub editor naweza kuwa editor ndivyo ambavyo katika taasisi na sisi tunaweza kufanya mabadiliko.
Lakini pia kuna wakati unafanya mabadiliko kwa faida lakini kuna wakati unafanya mabadiliko makubwa ya kuelekea mimi ni mwenyekiti mpya na viongozi wengine wapya kuna mahitaji ambayo tumeyaahidi mbele ya wanachama wangependa hayo mahitaji yafikiwe kwa hiyo wanaangalia mfano leo tangu Joketi ameondoka nafasi ipo wazi maana yake ni kwamba tunasubiri kuona mahitaji ya sasa yanahitaji mtu wa namna gani.
Lakini kuondolewa katika nafasi hakumaanishi mtu yule hafai yawezekana alikuwa hayuko vizuri kwenye nafasi hiyo lakini ipo nafasi nzuri zaidi ambayo inamtosha.
Ukirejea katika utaratibu wetu wa kazi kukaimu nafasi inamaanisha nafasi ambayo si yako kwa hiyo kipindi hicho waliona nafasi hiyo haina mwenyewe, hivyo wakamchukua Joketi wakamuweka na kukaimishwa lakini hakuthibitishwa ni kitu cha kawaida kama taasisi na naona huko aliko anafanya vizuri pengine kuliko alipokuwa kwetu na tumuombee afanye vizuri zaidi.
Swali: Unauzungumziaje uchaguzi uliokuweka madarakani uliuonaje?
Jibu: Uchaguzi wa mwaka 2017 ulikuwa mgumu, mgumu kabisa mimi nilikuwa kiongozi wa kata mpaka wilaya na nimeshiriki chaguzi nyingi lakini ule ulikuwa mgumu niishie kusema hivyo tu… Ulikuwa uchaguzi mgumu.
Swali: Pengine kupita kwako inaonyesha kwamba ulikuwa competent?
Jibu: I am not that competent isipokuwa kura tu ziliamua. Niligombea na watu wenye uwezo na ndiyo maana waliweza kupita mchujo wote lakini kura tu ndizo zilizoamua. Mimi niliwazidi wenzangu kura tu, lakini sikuwazidi uwezo. Uwezo wote wanao na hata huko walipo wanaendelea kufanya vizuri kwa uwezo uleule waliokuwa wameamini nao.
Swali: Umewahi kunukuliwa kuwa Tanzania hakuna upinzani na kumtaja Julius Malema wa Afrika Kusini ndiyo mpinzani wa kweli je, hilo limekaaje na huoni kama wapinzani nchini wanaminywa?
Jibu. Kuzungumza kuminywa ni kutafuta kivuli cha kujificha tu katika nchi ambayo demokrasia ipo wazi Tanzania tunayo kubwa. Kwa nini nilisema wapinzani Watanzania bado; wapinzani wa Tanzania hakuna hoja umejikita katika matukio ikitokea jambo upinzani unauona, lakini lile jambo likiisha ile nguvu inapotea lakini huku wamesajiliwa kuwa ni vyama vya siasa vyenye ajenda za kudumu na ajenda zao ni mbadala ya zilizopo katika chama kinachoongoza na kwamba hakuna ajenda zinazofanana.
Lazima ACT atatofautiana na Chadema from Januari to Desemba kwa sababu gani wote wamesajiliwa kwa sera tofauti sasa haiwezekani mnatofautiana kwa usajili kwa itikadi kisha mnaamua kutotofautiana kwa namba hiyo mmeamua kuacha kutofautiana kwa misingi hiyo sasa mnatofautiana kwa matukio. Tulitarajia kama sera ya Chadema ndiyo sera mbadala ya CCM inatakiwa kuwa hivyo from Januari to Desemba kama sera ya uchumi au afya wanayoiamini Chadema ni hii, lakini sasa kilichopo tuna mashindano ya matukio ya 1.5 trilioni na Mange Kimambi.
Kuna siku nchi hii itakosa matukio hatutakuwa na upinzani hilo ni jambo la hatari sana.
Swali: Unawezaje kulinganisha mazingira ya Tanzania na Afrika Kusini, huoni kama wapinzani wa Tanzania wamebanwa?
Jibu: Wamebanwa kwa nini? Afrika Kusini wanaamini katika kuchagua kwa kura na sisi tunawachangua viongozi wetu.
Lakini wao rais anaingia bungeni na huku Waziri Mkuu anakuwa criticize bungeni the same thing ni namna watu wanatumia platform vipi. Ni mara ngapi wapinzani wanaivua nguo Serikali bungeni nani aliwahi kuwaambia wanyamaze. Kwa hiyo uhuru ambao uko Afrika Kusini ni sawa tu uliopo hapa, lakini ni waambie tu uhuru usiyokuwa na mipaka ni utumwa. Uhuru wako unaanza pale uhuru wa mwingine unapoishia. Kwa mfano hapa Mwananchi kwa kuwa mnaruhusu basi mrekodi harusi mpaka chumba cha fungate hilo haliwezekani lazima tuwe na mipaka
Swali: Kabla hujachaguliwa kulikuwa na madai ya malimbikizo ya watumishi wa UVCCM je, wameshawalipa?
Jibu: Kimsingi mimi naamini mshahara wa watumishi ni haki yake na si sadaka. Ndiyo sababu umewekewa utaratibu lakini kama taasisi ina changamoto zake mipango na mikakati ni kuhakikisha watumishi wanapata mishahara kwa wakati lakini inapotokea wakakosa kwa wakati siyo lengo.
Hakuna mtu anayeweza kukwambia kwamba amekaa miaka 10 bila kupata mshahara ila atakwambia amecheleweshewa. Kucheleweshewa ni tofauti na kutokulipwa. UVCCM na CCM huwezi kusikia mtu halipwi. Hii inatokana na vyanzo tulivyonavyo havijaingiza fedha kwa wakati lakini haki na stahiki ile inabaki kuwa stahili ya mtumishi ingawa hatupendi itokee.
Swali: Umeingia katika kipindi cha mabadiliko ya CCM vyanzo vya mapato vinasimamiwa makao makuu badala ya kuwa kwenu, hali ikoje sasa?
Jibu: Kimsingi baraza la wadhamini la CCM ndilo limebeba dhamana ya mali zote, lakini usimamizi umebaki kuwa jumuiya husika kwa hiyo wamiliki wamebadilika lakini wasimamizi wamebaki walewale. Tumebaki na ile haki ya kusimamia mali zetu.
Swali: Arbert Msando aliwahi kunukuliwa akisema kwamba hamkumweleza ukweli mwenyekiti kuhusu idadi ya wanachama wenu hili limekaaje?
Jibu: Sisi hatuwajibiki kwa Msando, tunawajibika kwa mwenyekiti Taifa. Hatuwezi kuwa tunamjibu kila mtu. Tukiulizwa na vikao halali tutawaeleza na siwezi kuwa namjibu yoyote nawajibu leo Mwananchi kwa sababu ni chombo cha habari kina wajibu wa kufikisha taarifa kwa wananchi.
Lakini, by the time analizungumza lile jambo Msando ndiyo alikuwa anajiunga katika chama je, tuna uhakika gani alipewa taarifa sahihi na je, ni lini alipata hizo taarifa za UVCCM? Sijui msingi wa hoja yake lakini niseme tu kwa maana ya data za wanachama na kadi taasisi inajua msingi wa idadi inaanza katika kata. Ni ngumu sana kwa mwanachama aliyejiunga siku hiyo hiyo akapata idadi ya wanachama kuliko waliokuwepo.
Swali: Umepita nchi nzima kwa ziara mbalimbali lakini kwa upande huu wa pili kumekuwa na kamatakamata huoni kama kuna upendeleo?
Jibu: Upendeleo sijui mimi nafuatilia sana namuona Lema, Zito na Mbowe wote wanafanya siasa kila mtu anafanya na kielelezo ni leo Mbowe ameenda Mbeya unafikiri ataishia gerezani tu? Wasiotaka kutimiza wajibu ndiyo wanaotaka uhuru usiyo na mipaka, tumeomba ridhaa kwa wananchi tumepewa majimbo na kata kila mmoja aende kwake akafanye kazi. Haiwezekani katika jimbo lako huna muda wa kwenda halafu unataka kuzunguka nchi nzima. Kuna siku moja nimewahi kusema haiwezekani kuna watu katika nchi hii anataka kuwa kama mbio za mwenge anataka kuzunguka nchi nzima kila kijiji, lakini huyo huyo mbunge anayesema amenyimwa kuzunguka kuna kata hajawahi kwenda lakini anataka apewe haki ya kuzunguka nchi nzima. Hatuwezi kukubali hilo wewe umeomba ridhaa ya ubunge wa Mwanakwerekwe nenda huko kwa miaka mitano. Siku chama chako kikiwa na shughuli ya kitaifa watakuomba utaenda lakini kiserikali inasema fanya kazi yako.
Watu wanaonja katika majimbo yao halafu wanataka kula nchi nzima haiwezekani. Tunachofanya sasa ni kuwawajibisha kwa watu wao na ni lazima maana ukiwaambia kwa hiari hawafanyi.
Swali: Vipi siasa vyuoni tumeshuhudia mkiwaandaa vijana hili limekaaje?
Jibu: Hatujawahi kufanya siasa vyuoni isipokuwa wanafunzi waliopo vyuoni wanajihusisha na matawi yaliyokuwepo karibu na vyuo. Kujiunga na siasa ni haki yake ya kikatibu ila kwa taratibu za kishule hawaruhusiwi lakini wana haki ya kujiunga wanapotoka nje.
Kama kweli wapo wanaofanya chuoni hiyo ni hatari wanaruhusiwa kufanya nje tu na uzuri ni kwamba vyuo vipo na vinajua utaratibu.
Swali: Je, una mikakati gani?
Jibu: Kwanza ni kuwa mawakili wa kweli wa masilahi ya vijana nchini. Vijana wakiwa na mambo yao wajue kwamba kwa hili UVCCM ipo. Pia tunasimamia masilahi ya vijana, kuna haki, masilahi ya vijana hazitolewi. Leo kuna fedha asilimia tano kutoka kwenye halmashauri, je zinatoka kweli kwa vijana?
Kuna haki za michezo, kuna maeneo yametengwa kwa ajili ya michezo, sisi ni wajibu wetu kufuatilia je hayo maeneo yapo au haki hiyo imeporwa kwa sababu eneo amepewa tajiri kwa sababu ana uwezo?
Ilani ya CCM imeelekeza, shughuli za ujenzi wa miradi vijijini wapewe vijana na wanawake, hivyo tunafuatilia kama kweli inatekelezwa au halmashauri zinatoa hizo kazi au kampuni za kizungu na kibeberu yanapewa kila kitu kufanya.
Leo tumeanzisha Tanzania ya viwanda, je, ni ipi nafasi ya vijana katika viwanda hivyo? Wameendelea kuwa manamba au wamepewa heshima ya kuwa wakurugenzi na mameneja wa viwanda hivyo?