Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zanzibar moja, mradi waacha alama

Mratibu wa mradi wa Amani Yetu, Mshikamano wetu, Almas Ali (katikati) akizungumza kuhusu mafanikio na kufungwa kwa mradi huo Unguja. Picha na Jesse Mikofu

Unguja. Wakati mradi wa kusuluhisha migogoro ya kisiasa kisiwani Zanzibar ukifikia ukingoni, umeelezwa kuacha alama kubwa za mshikamano baina ya vyama vya siasa na kuleta ustawi wa jamii.

Zanzibar mara kadhaa imekumbwa na machafuko ya kisiasa hususani nyakati za uchaguzi ambapo watu kadhaa wamepoteza maisha na wengine kubaki na vilema.

Jitihada mbalimbali zimekuwa zikifanywa kuleta suluhu ya amani na kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) ambayo inavihusisha vyama viwili vikuu vya siasa kisiwani humo vya CCM na ACT-Wazalendo

Hata hivyo, ili kuleta mshikamano zaidi baina ya jamii ya kisiwa hicho, Machi 2022 ulianzishwa mradi wa ulioitwa kwa jina la Amani yetu, Mshikamano wetu ambao ulivihusisha vyama vinne vya siasa vya CCM, CUF, ACT-Wazalendo na Chadema na viongozi wa dini.

Mradi huo wa Sh1.5 bilioni uliofadhiliwa na Umoja wa Ulaya, kutekelezwa na Konrad Adenauer Stiftung (KAS) Tanzania na Zanzibar na Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (Zafela) kwa ushirkiano mkubwa na Serikali.

Akizungumza leo Juni 20, 2023 mjini Unguja, Mratibu wa mradi huo, Almas Ali amesema mradi huo unatarajiwa kufungwa rasmi na Makamu wa Kwanza wa Rais Othman Masoud Juni 27, 2023.

“Katika kipindi cha miezi 19 ya utekelezaji wa mradi huu umeleta uelewa kwa watendaji wa kisiasa kupitia mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuwashirikisha katika mazungumzo kwa ajili ya kuimarisha uhusiano na kuaminiana hususani ndani ya vyama vya siasa,” amesema

Mradi huo unatekelezwa ukiwa ni mwitikio wa uzoefu wa migogoro ya kisiasa iliyodumu kwa muda mrefu na hali ya vuguvugu ambayo imekuwapo zaidi katika nyakati za uchaguzi.

“Ni kweli ii imekuwa ikiathiri ustawi wa jamii na pia michakato ya kisiasa visiwani hapa

Amesema kuwapo kwa mradi huo ni muendelezo kuchangia juhudi ambazo zinafanywa na wadau wengine ikiwemo serikali kumaliza migogoro na kuhimiza majadiliano miongoni mwa vyama vya siasa.

Meneja kiongozi, Maria Kayombo amesema licha ya mradi huo kufikia kikomo na kujivunia mafanikio yaliyofikiwa, bado kunahitajika jitihada za makusudi kuendelea kuleta amani kisiwani humo.

Amesema jambo ambalo ni la kujivunia ambalo limefanikiwa kwa kiasia kikubwa ni kuwakutanisha pamoja wananchi wa ngazi ya chini tofauti na viongozi wakuu pekee.

“Kitendo cha kuwakutanisha pamoja vyama vya siasa wa ngazi za chini, viongozi wa dini, tukaa tukajadili changamoto hizi ni hatua moja kubwa sana, lakini kupitia michezo sanaa ambavyo vimefanywa chini ya mradi huu vimeleta faraja na mshikamano mkubwa,” amesema

Nao baadhi ya wajumbe wa vyama vya siasa wamesema mshikamano uliopatikana hakuna budi kuendeleza na kuleta amani Zaidi.

“Hii ni hatua nzuri lakini ushauri wangu kukoma kwa mradi huu isiwe ndio kukoma kwa amani yetu, tuendele kushikamana na wadau wengine kuendelza miradi yenmye tija kama hii kwa taifa letu,” amesema mjumbe kutoka ACT-Wazalendo Othman Kombo.