Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wazazi ‘ubize’ na simu unavyoathiri malezi, makuzi ya mtoto wako

Muktasari:

  • Miongoni mwa vitu vinavyowatia unyonge watoto wengi hasa maeneo ya mijini, ni simu za mkononi za wazazi wao wakitaja kuwa zinachukua muda mwingi waliopaswa kupewa wao na hivyo kutokuwa na mahusiano ya karibu ‘bond’ baina yao.

Dar es Salaam. Wakati tukisherehekea Siku ya Mtoto wa Afrika, imeelezwa kuwa wazazi kutumia muda mwingi kwenye simu hupunguza muda wa kuzungumza, kucheza au kuwajali watoto wao hivyo kuathiri malezi ya kihisia na ukuaji wa mahusiano ya karibu ‘bond’.

Hali imetajwa kuwa inaweza kuathiri maendeleo ya lugha kwa watoto wadogo, kwa kuwa wao hupata ujuzi wa lugha kupitia mazungumzo ya ana kwa ana, hivyo simu huchukua nafasi hiyo na kuchelewesha maendeleo ya lugha na mawasiliano.

Utafiti wa ‘The iPad Generetion’ – pediatric wa mwaka 2018 ulionyesha kuwa watoto huwa na hasira, huzuni au hata wivu wanapoona mzazi wao akiipa simu kipaumbele kuliko wao.

Utafiti huu ulionyesha kuwa wazazi wanaotumia simu kwa muda mrefu mbele ya watoto wao walisababisha watoto wao kuwa na tabia za kulalamika, kujisikia kupuuzwa na wakati mwingine kuwa na tabia za ukaidi.

Utafiti wa ‘Developmental Science’ uliofanywa na Dk Jenny Radesky ulibaini kuwa matumizi ya mara kwa mara ya simu wazazi mbele ya watoto wa umri mdogo, huathiri maendeleo ya kijamii na kihisia ya mtoto. Watoto walikuwa na matatizo ya kujieleza.

Mwaka 2019 Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitoa mwongozo wa kupunguza muda wa skrini kwa watoto na kusisitiza umuhimu wa mwingiliano wa moja kwa moja kati ya mzazi na mtoto (WHO guidelines on screen time for children).

Baadhi ya watoto (majina yanahifadhiwa) walioulizwa ni vitu gani hawavipendi kutoka kwa wazazi wao, simu ilitajwa mara nyingi zaidi.

“Sipendi mama anaposema hayupo nyumbani, lakini kumbe amejifungia ndani anaongea na kuperuzi kwenye simu yake,” amesema mtoto wa miaka minne.

Mtoto mwingine wa miaka 7 amesema, “Kuna wakati mama anasema anaumwa kichwa kumbe siyo kweli, anakuwa kwenye simu au Instagram anaperuzi, nikimfuata chumbani kwake naanza kuuliza maswali anasema hebu niache kichwa kinaniuma.”

Mtoto mwingine wa miaka 11 amesema baba yake hampi nafasi, “Ninapojaribu kukaa naye karibu kuzungumza naye anasema yuko bize, lakini hata kama hafanyi kitu anaangalia filamu nikijaribu kumshirikisha mambo yangu labda nina maswali, anasema niache kwanza naangalia movie (filamu) usinisumbue, hii tabia siipendi na inaniumiza.”

Mtaalamu wa saikolojia, Charles Nduku amesema wazazi wanapaswa kuwapa muda watoto wao na kuna nyakati wazazi wanatoa muda na watu baki na si watoto.

Amesema saikolojia ya mtoto hupenda kupewa muda na mzazi kwani ndiye anayemwamini na hutaka kusikilizwa wakati wote.

“Hata kama umechoka, vitu tenga dakika tano kila siku zungumza naye, atakupenda sana na kuona unamjali. Umri wa mtoto kuanzia mwaka 0 mpaka 17 wanahitaji kujaliwa sana kutoka kwa mzazi, vitu vingi anajikfunza kutoka kwako ukiwa bize na vitu vingine na si yeye inaanza kumwonyesha kwamba yeye si muhimu kuliko simu,” amesema.

Amefafanua kuwa hiyo ndiyo sababu ya watoto wengi kudai kuwa na simu katika umri mdogo wakiamini ni kitu muhimu sana.

Amesema hiyo ni pamoja na wazazi wanaowapatia simu watoto wao ili waendelee na mambo yao mengine.

“Elimu itolewe watu waelewe nini wanatengeneza kwa vizazi vyao, umuhimu na madhara ya hii kitu kinaweza kuleta athari gani baadaye, ikiwa mzazi na mtoto hawatajenga bond,” amesema.

Mtaalamu wa saikolojia, Karoli Mabula amesema moja ya kitu kibaya ambacho wazazi wanakosea ni kutowapa muda wa kusikiliza hisia zao.

“Ukifanya mazungumzo na mtoto wako utajua mambo mengi kumhusu, yanayomtatiza, anayoyafurahia na utajua namna ya kumsaidia. Kuna vitu vingi ambavyo watoto wanahitaji hasa katika malezi ya kisaikolojia,” amesema.