Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wazazi na wanafunzi wachangia sh64 milioni ujenzi miundombinu ya shule

Mkuu wa shule ya wavulana Tengeru boys, Gaudence Mtui akizungumza katika mahafali hayo mkoani Arusha.

Arusha. Wazazi wa  wanafunzi  wa kidato cha nne  na kidato cha pili wanaosoma katika Shule ya Sekondari ya  wavulana  Tengeru Boys iliyopo mkoani Arusha wamechanga kiasi cha sh64 milioni kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi wa mitihani ambapo kiasi kinachohitajika ni sh1.344 bilioni kukamilisha jengo hilo.

Fedha hizo zimeainishwa Septemba 30, 2024 mkoani Arusha na Mkuu wa shule ya  wavulana Tengeru boys,  Gaudence  Mtui wakati akizungumza katika mahafali ya 17  ya wavulana Tengeru boys ambapo jumla ya wanafunzi 136 wamehitimu ikiwemo  mahafali ya nne ya wanafunzi wenye ulemavu Holy Ghost viziwi.

Mtui amesema kuwa mbali na wazazi hao kuchangia fedha hizo, pia mamlaka ya hifadhi ya  Ngorongoro imewachangia kiasi cha sh15 milioni  kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo ambapo linatarajia kuanza hivi karibuni na litaweza kuhudumia wanafunzi  mia mbili kwa wakati mmoja na kuondoa changamoto wakati wa kufanya mitihani.

"Jengo tulilokuwa tukitumia ni dogo  kulingana na idadi kubwa ya wanafunzi iliyopo sasa hivi hivyo kukamilika kwa ujenzi huo utasaidia sana wanafunzi hao kuweza kutumia jengo hilo kwa ajili ya mitihani ambapo ukumbi huo utakuwa na ofisi nne na madarasa sita."amesema

Aidha amewataka wadau mbalimbali kusaidia juhudi hizo zilizoanzishwa na wazazi kwani wameonyesha mfano wa kuigwa kwa ajili ya kusaidia watoto wao kuwa na ukumbi huo.

Mtui amesema kuwa, kumekuwepo kwa kiwango kikubwa cha ufaulu shuleni hapo ambapo mitihani ya Mock na CSSC  ambayo walifanya kikanda vijana wote walishika nafasi ya kwanza katika kanda ya kaskazini Magharibi inayojumisha mikoa ya Kulima,Arusha na Manyara.

Ameongeza kuwa, kwa upande wa shule ya Holy ghost viziwi walimu wanajitahidi sana wakiamini  kuwa ulemavu sio kizuizi cha kufikia ndoto  ya mafanikio kwa vijana wetu wasiosikia, ambapo wahitimu wamekuwa wakipata daraja la kwanza mpaka daraja la tatu na vijana wote waliomaliza kidato cha nne  kati.ya 2021, 2022 na 2023 walifanikiwa kuendelea na masomo katika ngazi zingine za kitaaluma kama kidato cha tano na vyuo vya kati.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika mahafali hayo  Kamishna msaidizi mwandamizi mamlaka ya hifadhi Ngorongoro, Dk Mariamu  Kobelo  amesema, shule hiyo imekuwa ikiwalea watoto na kuwafundisha malezi mazuri ya kiroho sambamba na kuwafundisha kuhusu suala zima la maadili na kuweza kuepukana na vitendo viovu  hususani wanapokuwa mtaani.

Amesema kuwa, kila mmoja anashuhudia namna ambavyo kumekuwepo na mmomonyoko  wa maadili unaosababishwa na utandawazi, hivyo amewaomba wazazi wajitahidi kuwa karibu na watoto wao kwa sababu safari ya maisha imeanza .

"Nawaomba sana wazazi mhakikishe mnawajengea watoto mazingira mazuri ya elimu kwa sababu ndio urithi pekee unaoweza kumpatia mtoto kwa ajili ya maisha yake ya baadaye"amesema Mariamu.