Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watu 17 wamenusurika kusombwa na maji mkoani Kilimanjaro

Wananchi kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Kilimanjaro wakiondoa magogo katikati ya Barabara Kuu ya Dar es salaam – Moshi - Arusha, eneo la Kiboriloni Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro leo Jumanne Mei 6, 2025.

Moshi. Watu 17 wanaoishi Kata ya Kiboriloni, Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, wamenusurika kusombwa na mafuriko baada ya nyumba zao kuzingirwa na maji usiku wa kuamkia leo.

Tukio hilo limetokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Mafuriko hayo yamesababishwa na kujaa kwa Mto Kisangiro kufuatia mvua kubwa zinazonyesha katika maeneo ya milimani.

Wananchi kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Kilimanjaro wakiondoa magogo katikati ya Barabara Kuu ya Dar es salaam – Moshi - Arusha, eneo la Kiboriloni Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro leo Jumanne Mei 6, 2025.

Mvua hizo zimesababisha mto huo kusomba magogo na takataka, hali iliyosababisha daraja la Mto Kisangiro lililopo kwenye barabara kuu ya Moshi–Arusha–Dar es Salaam kuziba. Kutokana na kuziba huko, maji yalifurika juu ya daraja na kutapakaa hadi katika makazi ya wananchi.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Hata hivyo, kwa sasa barabara hiyo haipitiki kutokana na magogo na tope lililosababishwa na mafuriko, ambayo yameziba njia hiyo.

Akizungumza na Mwananchi leo, Mei 6, 2025, Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi, amesema kuwa watu 17 wameokolewa baada ya nyumba zao kuzingirwa na maji kufuatia mafuriko, na hadi sasa hakuna kifo kilichoripotiwa.

Kamanda Mkomagi, ambaye yupo katika eneo la tukio, amesema jeshi hilo kwa kushirikiana na wananchi linaendelea na juhudi za kuondoa magogo yaliyokwama barabarani ili kufungua njia na kuruhusu magari kupita.

"Saa 7:50 usiku tulipokea taarifa za mafuriko yaliyozingira nyumba kadhaa katika eneo la Kiboriloni, tulifika kwa haraka na kufanikisha uokoaji wa watu 17," amesema Kamanda Mkomagi.

Ameongeza kuwa "Daraja la hapa Kiboriloni lilizibwa na taka pamoja na magogo yaliyoshushwa kutoka milimani, hali iliyosababisha maji kukosa njia ya kupita na kuingia kwenye makazi ya watu."

Kamanda Mkomagi, amesema madhara yaliyosababishwa na mafuriko hayo ni uharibifu wa mali na miundombinu ya barabara na kwamba hakuna majeruhi au vifo vilivyoripotiwa hadi sasa.

Amesema  kazi ya kuondoa taka na magogo inaendelea katika eneo hilo kwa kushirikiana na wananchi ili barabara hiyo iweze kupitika.


Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi.