Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watu 13 wafariki ajalini Songea

Mkuu wa Wilaya, Songea Wilman Ndile

Dar es Salaam. Watu 13 wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa kwenye ajali ya gari la mnada aina ya Fuso katika Kijiji cha Namatuhi wilayani Songea mkoani Ruvuma wakitokea Ndongosi Mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.

Akithibitisha kutokea tukio hilo Mkuu wa Wilaya, Songea Wilman Ndile amesema ajali hiyo ilitokea jana usiku baada ya gari hilo lililokuwa limebeba wafanyabiashara kuteleza na kutumbukia mtoni.

“Maiti nyingi ni za mjini hapa Lizaboni, Ruvuma na Majengo. Maiti hizo zimehifadhiwa kwenye Hospitali ya Mkoa kwa utambuzi zaidi. Viongozi wanakutana saa nne na watatoa taarifa kamili.” Amesema DC Ndile


Kwa habari zaidi endelea kufuatilia Mwananchi na mitandao yake.