Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watatu wasimamishwa kazi kuchelewesha huduma hospitalini

Muktasari:

  • Ujumbe wa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu umewasimamisha kazi watumishi watatu wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Tanga, Bombo Tanzania wamesimamishwa kazi huku wengine 26 wakichunguzwa baada ya kudaiwa kukwamisha utoaji huduma na kwenda kufanya kazi katika hospitali binafsi muda wa kazi.

Dar es Salaam. Ujumbe wa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu umewasimamisha kazi watumishi watatu kupisha uchunguzi na wengine 26 kutoka idara mbalimbali wakiendelea kuchunguzwa kwa kile kinachoelezwa kukwamisha utoaji huduma kwa wananchi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga – Bombo.

Ujumbe huo ukiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel umefanya maamuzi hayo leo Oktoba 20, 2023 wakati akizungumza na uongozi wa hospitali hiyo wakati wa ziara yake ya siku moja kufuatilia maelekezo ya waziri kuhusu kero kwa wananchi wa Tanga kutopata huduma nzuri za afya.

Dk Mollel amesema watumishi watatu waliosimamishwa kazi ni daktari bingwa wa mifupa, mtaalamu wa usingizi na muuguzi wa chumba cha upasuaji.


“Tunaendelea kufanya uchunguzi katika idara zote za Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga – Bombo na watumishi wengine 26 wanaendelea kuchunguzwa,” ameeleza Dk Mollel.

Dk Molel ametoa onyo kali kwa madaktari wote nchini wenye tabia za kutoa rufaa kwa wagonjwa bila sababu za msingi za matibabu kutoka kwenye ospitali za Serikali na kuwapelekea kwenye hospitali binafsi.

Aidha, amesema wamiliki wa hospitali binafsi wanatakiwa kufuata taratibu na kanuni zilizopo katika kuendesha hospitali zao kwani yeyote atakayebainika kuwarubuni madaktari wa hospitali za Serikali kutoa rufaa bila sababu ya msingi ya kimatibabu watachukuliwa hatua za kisheria.

“Siyo kwamba tunawakataza madaktari wa Serikali kufanya kazi baada ya muda wa serikali kuisha lakini isiwe muda wao wa kazi wanakwenda kufanya kazi kwenye hospitali binafsi na kusababisha wagonjwa kutopata huduma katika hospitali za serikali,” amesisitiza Dk Mollel.

Dk Mollel ametoa rai kwa watumishi wa afya nchini kuhakikisha wanazingatia miiko na maadili ya viapo vya taaluma zao ili kuhakikisha wanaleta ubora wa huduma katika hospitali zote nchini.

Vilevile ametumia fursa hiyo kuwakumbusha watumishi wa afya nchini kuwa kipaumbele cha Rais Samia Suluhu Hassan ni ubora wa huduma za afya kwa wananchi wote bila kujali hali zao za kiuchumi.