Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watanzania waonywa uchaguzi usiwe kisingizio cha kuvuruga amani

Waumini wa dini ya Kiislamu mkoani Dodoma wakiwa wanashiriki swala ya Eid Al-Adha katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo Jumamosi Juni 7, 2025. Picha na Edwin Mjwahuzi

Muktasari:

  • Tanzania inatarajia kufanya uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani Oktoba, 2025.

Dodoma. Watanzania wametakiwa kuwa na subira kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba, 2025 na kuiombea nchi amani kwa kuwa baadhi ya watu wanaweza kutumia kipindi hiki kuvuruga amani iliyopo.

Sheikh Yahya Kivuma amesema hayo baada ya swala ya Eid El -Adh'haa iliyofanyika kiwilaya katika Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma leo Juni 7, 2025.

Amesema katika kipindi hiki kutakuwa na maneno mengi ambayo yanaendelea kwa kisingizio ni mwaka wa uchaguzi, ili kuvuruga amani ya nchi.

Waumini wa dini ya Kiislamu mkoani Dodoma wakiwa wanashiriki swala ya Eid Al-Adha katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo Jumamosi Juni 7, 2025. Picha na Edwin Mjwahuzi

“Nawaomba Watanzania tuiombee nchi yetu amani katika kipindi hiki maana amani ikipotea hatuna nchi nyingine ya kukimbilia, tuna nchi moja tu ya Tanzania. Kwa hiyo, tuilinde amani tuliyonayo maana ikipotea ni gharama kuirudisha,” amesema.

Sheikh Kivuma amewataka Watanzania kuwaombea viongozi walioko madarakani ili wawe na busara ya kuiongoza nchi.

Sheikh Swedi Twaibu aliyemwakilisha Mufti katika swala hiyo, amewataka Watanzania kuwa na subira na kuvumiliana kwa sababu ni mwaka wa uchaguzi, hivyo watu wengi watatumia nafasi hiyo kuvuruga amani.

Waumini wa dini ya Kiislamu mkoani Dodoma wakiwa wanashiriki swala ya Eid Al-Adha katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo Jumamosi Juni 7, 2025. Picha na Edwin Mjwahuzi

Amesema mwaka huu kuna watu watavuana nguo kwa kutoleana siri zilizofanyika miaka ya nyuma kwa sababu tu ya uchaguzi, hivyo amewaomba Watanzania kuwa wavumilivu.

“Kutakuwa na mambo mengi yanayoendelea nchini kikubwa tuwe wavumilivu na subra kwa sababu kila mtu ana mambo anayoyapitia. Pia tusisahau kuwaombea viongozi wetu kwa kuwa wanapitia mambo mengi na wengine wanawaita majina mabaya kwa sababu ya kuharibiana kuelekea uchaguzi mkuu,” amesema.

Mkazi wa Jiji la Dodoma, Twaha Kivale amesema sikukuu imekwenda vizuri kwani wameswali kwa amani na utulivu.

Amewataka Watanzania kusherekea sikukuu kwa amani pamoja na familia zao na kujiepusha na mambo yatakayohatarisha maisha yao.