Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watanzania wahimizwa kupiga kura za World Travel Awards

Meneja Masoko TTB, Vivian Temi akizungumza na vyombo vya habari

Muktasari:

  • Kura tuzo za kimataifa za World Travel Awards 2025 zinazotarajiwa kufanyika Julai 28, 2025 Tanzania zimeanza kupigwa na pazia lake litafungwa Mei 4, 2025.

Dar es Salaam. Pazia la kupigia kura vivutio vya utalii vya nchi vilivyoteuliwa kushiriki katika tuzo za kimataifa za World Travel Awards 2025 limefunguliwa rasmi,huku Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), ikiwahimiza watanzania kupiga kura kwa wingi.

Machakato huo umefunguliwa ukiambatana na kampeni ya “Tanzania Shines 2025”, kuhamasisha watanzania kushirki kikamilifu ili nchi ishinde tuzo hizo za Kimataifa zina lengo la kutambua mchango wa wadau katika Sekta ya Utalii na Ukarimu Duniani, zinatolewa na kampuni ya World Luxury Media Group.

Tuzo hizo zinatajiwa kufanyika Dar es Salaam, Julai 28,2025 na Tanzania pamoja na kuwa mshiriki lakini imepewa heshima ya kutangaza washindi wa kanda hiyo, ijulikanayo kama Africa & Indian Ocean Gala Ceremony.         

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meneja Masoko wa TTB, Vivian Temi amesema kuwa tuzo hizo zimekuwa zikitolewa kwa zaidi ya miaka 30, zikilenga kutambua mafanikio ya wadau wa utalii na ukarimu duniani kote.

Katika mwaka 2024, Tanzania ilifanikiwa kuibuka na tuzo mbalimbali zikiwemo World’s Leading Safari Destination, Africa’s Leading Destination, Africa’s Leading Tourist Board (TTB), Africa’s Leading Tourist Attraction – Mlima Kilimanjaro na Africa’s Leading National Park – Serengeti

Amesema kwa mwaka huu 2025, Tanzania imeteuliwa  kushiriki katika vipengele 14 na kuomba Watanzania Kila mmoja kuingia World Travel Awards na kuichagua Tanzania.

Miongoni mwa vipengele inavyowania ni Africa’s Leading Destination, Africa’s Leading National Park – Serengeti, Leading Tourist Attraction – Mlima Kilimanjaro na Ngorongoro, Leading Beach Destination – Zanzibar, Bandari bora Africa Bandari ya Dar es Salaam, Uwanja Bora wa ndege Julius Nyerere Na mbuga nyingine kama Nyerere, Tarangire, Kitulo, Katavi, na Mahale zikiwakilisha katika vipengele vya kipekee.

Pia, kampuni mbalimbali za huduma za utalii kama vile Zara Adventures, Gosheni Safaris, Gran Meliá, na Serena Hotel nazo zimetajwa kuwania tuzo.

“Kwa pamoja, tunapaswa kutumia nafasi hii kuonyesha uzalendo wetu kwa kupiga kura na kuitangaza Tanzania kama nchi ya kipekee kwa vivutio vya asili, utamaduni, na ukarimu,” amesema.

Kampeni ya “Tanzania Shines 2025” itafanyika nchi nzima kwa njia ya redio, televisheni, mitandao ya kijamii, na kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali. Shughuliya  kupiga kura kwa ukanda wa Afrika na Bahari ya Hindi linatarajiwa kufungwa Mei 4, 2025.

Kulingana na Vivian amesema utaratibu wa kupiga kura unaenda www.worldtravelawards.com/vote na inabidi mpigaji ajisajili na kurudi kwenye sanduku kukubali na kwenda jukwaa la tuzo kisha kupiga kura.

Mafanikio Tanzania kuingia katika tuzo hizo yanachagizwa na juhudi za pamoja za Serikali, wadau wa utalii, na kampeni za kimataifa kama filamu ya Rais Samia Suluhu Hassan, The Royal Tour, ambayo imeongeza umaarufu wa vivutio vya Tanzania duniani kote.