Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ludewa yasaini mkataba wa upangishaji wa vizimba vya samaki

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Wise Mgina akiwa na wawekezaji wakisaini makubaliano ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba wilayani Ludewa.

Muktasari:

  • Lengo la mradi huo ni kukuza uchumi wa wilaya hiyo na kupambana na udumavu kwa kuongeza upatikanaji wa protini.

Njombe. Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa imesaini mkataba na wawekezaji kwa ajili ya kupangisha vizimba vya ufugaji wa samaki katika Ziwa Nyasa, ikiwa ni sehemu ya kukuza uchumi na kupambana na udumavu wilayani humo.

Hayo yamesemwa leo, Aprili 25, 2025 na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Wise Mgina, wakati wa kusaini mkataba huo uliofanyika katika ofisi ya mwenyekiti huyo huko wilayani Ludewa Mkoa wa Njombe.

Amesema mradi huo wa ufugaji wa samaki kupitia vizimba utafanyika katika kata za Iwela, kijiji cha Iwela eneo la Chuva pamoja na Uhonjo katika kata ya Lupingu wilayani Ludewa.

Amesema mradi huo unalenga kutumia eneo la Ziwa Nyasa lenye ukubwa wa mita za ujazo 21.4 kwa ajili ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba, ikiwa ni sehemu ya halmashauri hiyo kukuza uchumi wa wilaya hiyo.

"Hii ni sehemu ya juhudi za halmashauri yetu katika kukuza uchumi wa wilaya na kupambana na udumavu kwa kuongeza upatikanaji wa protini kupitia samaki," amesema Mgina.

Amewashukuru wawekezaji, hususan wazawa wa wilaya hiyo, kwa kuona umuhimu wa kuwekeza nyumbani, kwani uwekezaji huo utasaidia kuleta maendeleo kwa wananchi wilayani Ludewa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Sunday Deogratias, amesema mradi huo utakuwa chachu kwa wananchi wengine kuona umuhimu wa kuwekeza nyumbani.

"Mradi huu utasaidia kuitangaza halmashauri sehemu mbalimbali nchini, hivyo itaongeza uchumi wa wilaya, mkoa, na hata Taifa kwa ujumla," amesema Deogratias.

Mmoja wa wawekezaji hao wa vizimba vya samaki, Stanley Gowele, amesema wamejipanga kikamilifu kutekeleza mradi huo na kuomba ushirikiano kutoka kwa uongozi wa halmashauri na wananchi ili kuhakikisha mradi huo unakuwa na tija kwa wote.

"Tunaomba tushirikiane kwa pamoja ili kuongeza thamani ya mradi unaokwenda kuutekeleza. Tupo tayari kusaini mkataba na kuanza kazi mara moja," amesema Gowele.