Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wataka wagombea wadhalilishaji kuenguliwa kwenye uchaguzi

Muktasari:

  • Wakati Serikali imewasilisha miswada ya kufanya marekebisho katika sheria za uchaguzi na ile ya vyama vya siasa, wadau wa masuala ya wanawake wametaka marekebisho hayo yakite katika kuondoa vikwazo vinavyowafanya wanawake wengi washindwe kushiriki katika siasa.

Dodoma. Wadau wa masuala ya wanawake wamependekeza kuwekwa kwa kifungu katika sheria za uchaguzi kitakachowaengua wagombea watakaothibitika kujihusisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia na udhalilishaji wakati wa chaguzi ili kuwavutia wanawake wengi kushiriki katika siasa.

Wameyasema hayo katika mkutano wa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na  Muungano wa Wabunge wanawake uliolenga kujadili mapendekezo ya marekebisho ya Sheria za Vyama vya Siasa, Sheria ya Taifa ya Uchaguzi na Sheria ya Gharama za Uchaguzi na Ukatili dhidi ya wanawake katika siasa.

Semina hiyo iliandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF), Shirika la Fredrich Ebert Stiftung (FES) na Taasisi ya Kimataifa ya Marekani inayojihusisha na masuala ya demokrasia (NDI).

Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa WiLDAF, Anna Kulaya amesema utafiti walioufanya umeonyesha kuwa wanawake wengi wamekuwa wakifanyiwa ukatili katika siasa lakini ukatili huo unakuwamkubwa sana wakati wa mzunguko wa uchaguzi.

“Wanawake wamekuwa wakikutana na udhalilishaji, wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya rushwa ya ngono. Wamekuwa wakifanyiwa vitendo vingi ambavyo vinadhalilisha utu wao,”alisema.

Amesema hivyo wanategemea marekebisho ya sheria ya uchaguzi kufafanua vitendo vya ukatili wa kijinsia hususani ukatili wa wanawake wakati wa uchaguzi kuanzia ndani ya vyama.

Kulaya amesema sheria hiyo itoe mbinu mbalimbali za kukabiliana na hivyo vitendo ili kuruhusu wanawake wengi kushiriki katika masuala ya uchaguzi.

“Sheria iweke Mgombea yoyote atakayebainika kuwa ametenda vitendo vya ukatili wa kijinsia, ametenda vitendo vya ukatili wa jinsia au wakati wa uchaguzi kiwe kigezo kimojawapo cha kuondolewa katika nafasi yake ya ugombea,”amesema.

Amesema kwa kufanya hivyo kutaondoa vitendo vya udhalilishaji, ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake vilivyokuwa vikijitokeza na kukatisha wanawake wengi kuingia katika ulingo wa kisiasa.

Naye Mbunge wa Viti Malum (CCM), Neema Lugangira amesema jambo kubwa ambalo atalibeba ni kuhakikisha kuwa asilimia kubwa ya wagombea katika chaguzi kuu mbili wanakuwa wanawake.

“Kwasababu ili mtu uweze kugombea katika ngazi za kikata, kitongoji jimbo lazima awe na vyama vya siasa. Unaweza ukaweka mazingira mazuri kama hakuna takwa la kisheria lazima wateue asilimia fulani hatutaweza kufika,”amesema.

Amesema kikubwa ni kusaidia jamii kubadilisha mitazamo katika suala la wanawake na uongozi na kuhamasisha wanawake wengi kujitokeza kugombea katika chaguzi zinazokuja.


Yaliomo na yasiyokuwemo 

Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria (OUT) Dk Victoria Lihiru amesema  miongoni mwa mambo mazuri yaliyomo katika miswada ya Sheria za uchaguzi ni ujumuishaji wa makundi, kutaka vyama vya siasa kuwa na mipango wa kuimaimarisha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika masuala ya uchaguzi.

“jambo lingine ni kuhakikisha katika vyombo vya siasa ambavyo vinatatua migogoro mbalimbali watu wanaokaa kwenye ngazi ya kwanza ya utatuzi hawatakiwi kukaa kwenye ngazi ya rufaa ya vyombo hivyo,”amesema.

Amesema jambo kingine katika muswada hiyo ni kuwa na dawati la ujumuishaji wa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika masuala.

Dk Victoria amesema mapungufu ambayo wamekuwa wakiyapendekeza ikiwemo Sheria ya Vyama vya Siasa kuweka kiwango maalum cha vyama siasa wanapokuwa wanachagua viongozi wao.

Amesema mapungufu mengine ni vyama vya siasa kulazimishwa kuweka kiwango cha wanawake watakaowateua katika kugombea kwenye nafasi mbalimbali za uongozi na kutoa mfano katika uchaguzi wa mwaka 2020 vyama vya siasa nchini viliteua asilimia tisa ya wanawake kugombea kwenye uchaguzi.

“Changamoto nyingine ni kuweka mipango dhabiti na kuweka motisha na adhabu ambazo ziko imara katika kuhakikisha vitendo vya ukatili wa wanawake katika uchaguzi na kwenye harakati za kisiasa vinakatalikwisha,”amesema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk Anna Henga amesema suala la 50 katika uongozi wa kisiasa ni muhimu sana na hivyo vyama vinatakiwa kupewa ulazima katika kulifikia hilo.

“Vyama vipewe ulazima katika sheria kuwa katika kila ngazi ya uongozi kuwe na asilimia 50 kwa 50…Hii itasaidia kufikia 50 kwa 50 hadi katika ngazi ya kitaifa,”amesema.

Amesema iwekwe katika katiba, kanuni, sera namna ya upatikanaji wa watu wa kuwapata hiyo 50 kwa 50 kwenye nafasi za uongozi.

Pia alipendekeza vyama vilazimishwe angalau asilimia 30 ya ruzuku inakwenda katika makundi ya wanawake, vijana na wenye ulemavu ili kuzuia wanawake wengi kushindwa kugombea sababu ya kushindwa kumudu gharama za uchaguzi.


Watakiwa kujitokeza kutoa maoni yao

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Dk Joseph Mhagama amesema kwa kuwa bado Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson hajapanga kamati za kwenda kufanya uchambuzi wa miswada ya sheria za uchaguzi iliyowasilishwa jana , wadau mbalimbali wakiwemo wabunge wanatakiwa kujitikeza kutoa maoni yao katika kamati za Bunge zitakazopelekewa miswada hiyo.

“Niwaambieni waheshimiwa wabunge kule kwenye kamati ndipo kunafanyika kazi kubwa za uchambuzi, kwa hiyo mheshimiwa Spika atakapotaja kamati zitakazoichambua basi mjitokeze kutoa mapendekezo yenu kuhusu sheria hizi,”amesema Dk Mhagama.