Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Washikiliwa wakidaiwa kulawiti zaidi ya wanafunzi 10 Monduli

Muktasari:

  • Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Joshua Nassari amesema wanafunzi hao hawajafanyiwa vitendo hivyo vya ukatili shuleni, bali wamefanyiwa kwa nyakati tofauti nje ya shule wakiwa wanachunga mifugo ambapo baadhi ya wahusika wa vitendo hivyo ni ndugu wa wanafunzi hao na wanatoka 'boma' moja.

Arusha. Jeshi la Polisi mkoani Arusha linashikilia watu kadhaa wanaodaiwa kwa nyakati tofauti kuhusika na vitendo vya ulawiti kwa wanafunzi wa kiume zaidi ya 10 wanaosoma madarasa tofauti katika shule moja ya msingi wilayani Monduli Mkoa wa Arusha.

Matukio hayo yanayodaiwa kufanyika kwa nyakati tofauti pindi wanafunzi hao wawapo machungani, ambapo baadhi ya waathirika wa tukio hilo wanadaiwa kufanyiwa vitendo hivyo na ndugu zao wa karibu kutoka 'boma' moja.

Akizungumzia tukio hilo leo Ijumaa Septemba 29, 2023, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo amesema wanashikilia watu kadhaa na kwa sasa hawezi kutaja majina wala idadi yao na wanaendelea kuwahoji na kuwa wanaoshikiliwa ni vijana wadogo wenye umri kati ya miaka 14 hadi 15.

"Tunawashukilia watu kadhaa na tunaendelea kuwahoji na tumegundua wote wako chini ya umri wa miaka 18, kwa hiyo kuna sheria na taratibu zake pia, hatuwezi kuwataja majina kwa sababu ya umri wao kuwa mdogo, naomba pia nisitaje idadi ya tunaowashikilia kwa sasa hadi tukamilishe uchunguzi," amesema.

"Kufuatia hii naomba jamii iwalee vizuri watoto kwani tunaowashikilia wanatoka boma (familia) moja na hao waathirika, kwa hiyo tukiwa na watoto hata kama ni ndugu, jamii iwe inawatazama kwani katika hili tukio unakuta kijana wa miaka 14 au 15 amemfanyia ukatili mwenzake wa miaka 11 au 12, wazazi wahusike kwenye malezi ya watoto wao," amesitiza Kamanda.

Aidha tukio hilo lilibainika baada ya baadhi ya wanafunzi kulalamika kwa walimu wao shuleni hapo, huku wengine wakidaiwa kuanza kuonyesha tabia zisizo za kawaida ikiwa ni pamoja na kuwaambia wanafunzi wenzao wa kiume kuwa wanawapenda.

Wakielezea tukio hilo baadhi ya wanafunzi hao ambao wanasoma darasa la tatu, nne na la tano wamedai kufanyiwa kitendo hicho kwa zaidi ya mara moja.

Mmoja wa wanafunzi hao,amedai kuwa akiwa machungani alishikwa na kijana ambaye alimpeleka kwenye pori na kumvua nguo zake kisha kumlawiti.

"Aliyenifanyia kitendo hiki ni mkubwa sisomi naye darasa moja alishamaliza shule na amekuwa akinifanyia hivyo mara kwa mara, kwa sasa nikienda kujisaidia haja kubwa wakati mwingine na damu inatoka, tunaomba msaada tuweze kupona na kuendelea na masomo kama kawaida," amesema mmoja wa wanafunzi anayesoma darasa la tatu shuleni hapo.



Mmoja wa wazazi ambaye amedai mtoto wake amefanyiwa kitendo hicho, ameeleza kuwa aliitwa shule kwenye kikao baada ya baadhi ya watoto kulalamika kwa walimu hivyo wakaenda na kubaini baadhi ya watoto wao kufanyiwa kitendo hicho.

Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Joshua Nassari alithibitisha kutokea  kwa matukio hayo ambapo amesema watoto hao hawajafanyiwa vitendo hivyo vya ukatili shuleni bali wamefanyiwa nje ya shule wakiwa wanachunga mifugo na kuwa suala hilo linaendelea kufanyiwa kazi.

"Watu wangu wanaendelea kuzifanyia kazi tunatafuta hao watu, hilo ni tukio la nyuma siyo tukio la juzi, linaonekana ni siku nyingi limefanyika sema taarifa hazikupatikana zimekuja kupatikana baada ya kufichuafichua huko kijijini, tumekuja kulipata sisi kuwapima na nini hata hiyo michubuko ukiitafuta kuipata ila kuna wengine wanaonekana wamefanyiwa ukatili huo," amesema Nassari.