Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kikwazo elimu ukatili wa kijinsia hiki hapa

Afisa maendeleo wilaya ya Chemba Pamela Gango akifungua mkutano wa hadhara wa kuelimisha wananchi dhidi ya ukatili wa kijinsia.

Muktasari:

Licha ya mkakati wa Serikali kutoa elimu dhidi ya ukatili wa kijinsia, imeelezwa kuwa dhana ya ‘kumalizana kinyumbani,’ hasa kwenye ya ubakaji, ulawiti na mimba za utotoni, imekuwa ikikwamisha juhudi za haki kupatika kwa whanga wa matukio hayo.

Dodoma. Licha ya mkakati wa Serikali kutoa elimu dhidi ya ukatili wa kijinsia, imeelezwa kuwa dhana ya ‘kumalizana kinyumbani,’ hasa kwenye ya ubakaji, ulawiti na mimba za utotoni, imekuwa ikikwamisha juhudi za haki kupatika kwa whanga wa matukio hayo.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Ijumaa September 8, 2023; Afisa Mradi Msaidizi kutoka asasi ya Counsenuth, Karim Kapama, amesema kuwa licha ya jitihada wanazofanya kuelimisha umma juu ya ukatili wa kijinsia, baadhi ya kesi zimekuwa zikimalizwa katika ngazi ya familia.

"Tumekuwa tukizunguka kwenye vijiji mbalimbali wilayani Chemba, kuelimisha wananchi juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia. Changamoto kubwa inayojitokeza ni kwamba wahanga wa matukio hayo wamekuwa hawapati haki wanayostahili kwani wazazi na walezi wamekuwa wakimalizana kinyumbani badala ya kwenda mahakamani," amesema Karim.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Wilaya ya Chemba Siwema Juma ameishukuru asasi ya Counsenuth kwa uelimishaji umma juu ya matukio ya ukatili wa kijinsia. Amewasihi kuendea na kampeni hiyo ya kutokomeza ukatili wa kijinsia wilayani humo.

"Kumekuwa na mabadiliko makubwa tangu Counsenuth waanze kuelimisha jamii. Tunaona wanaume wameanza kuelewa madhara yanayotokana na ukatili wa kijinsia. Na Imani huu utakuwa mwanzo wa usawa wa kijinsia," amesema.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Paranga, Asha Hamisi, amekemea vikali tabia ya kumalizana kinyumbani kwa makosa ya ukatili wa kijinsia yanayofanyika. Amesema hayo kwenye mkutano wa kuelimisha wananchi juu ya kupiga vita ukatili wa kijinsia.

"Unakuta mtoto anafanyiwa ulawiti au ubakaji lakini wazazi wanakaa kumalizana kinyumbani kwa kulipa fedha na mifugo kunyamazisha ukatili huo. Watu wanaendelea na matendo maovu kwa sababu uwezo wa kuukwepa mkono wa sheria," amesema.

Metilda Nicholas ambaye ni Ofisa Polisi, dawati la jinsia Wilaya ya Chemba, ameeleza kuwa kesi za ukatili wa kijinsia zimekuwa zikiishia njiani. Inapofika wakati wa kutoa ushahidi mahakamani, wahanga wa ukatili wa kijinsia wamekuwa wakiishia njiani.

"Tumekuwa tukitafuta taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia katika kaya mbalimbali. Kesi zinazobainika zimekuwa zikiishia njiani kwa kukosa ushahidi. Elimu kwa umma inahitajika ili kuwapa wananchi nafasi ya kujifunza njia sahihi ya kukabiliana na ukatili wa kijinsia"

Matukio hayo ya ulawiti, ubakaji na mimba za utotoni umehusishwa na ugumu wa maisha. Wananchi wamekuwa wakipokea, fedha na mifugo ili kunyamazia matukio ya ukatili wa kijinsia