Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wapiga simu zimamoto wakiomba kutafutiwa wachumba

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mwanza, Kamila Labani.

Muktasari:

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Mwanza limesema miongoni mwa sababu zinazopunguza ufanisi na kukwamisha shughuli za uokozi mkoani humo ni pamoja na baadhi ya watu kupiga simu namba 114 wakiomba kutafutiwa wachumba.

Mwanza. Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Mwanza limesema miongoni mwa sababu zinazopunguza ufanisi na kukwamisha shughuli za uokozi mkoani humo ni pamoja na baadhi ya watu kupiga simu namba 114 wakiomba kutafutiwa wachumba.

Akizungumza Julai 10, 2023 katika hafla ya kuwavisha vyeo askari 20 wa jeshi hilo waliopandishwa vyeo, Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mwanza, Kamila Labani ametaja changamoto nyingine kuwa ni baadhi ya watu kuomba kuunganishwa Freemason wapate utajiri.

Kamila ametaja changmoto nyingine ni mashuhuda na wahanga wa ajali za moto kuchelewa kutoa taarifa janga linapotokea huku, tabia ya baadhi ya watu kupiga wakitafuta wachumba na ujenzi holela wa makazi hasa maeneo ya milimani ndani ya Jiji la Mwanza kukwamisha magari na maofisa wa jeshi hilo kufika eneo la tukio.

Kufuatia changamoto hizo, Kamila amewataka wanaopiga simu hiyo kwa lengo la kufanya kejeli kutofanya hivyo kwani kunapoteza muda ambao ungetumika kutoa huduma na kupunguza madhara kwa wanaokutwa na majanga.

“Wako watanzania wenzetu anapiga simu halafu anauliza anataka kujiunga na Freemason, mwingine anauliza mambo ya ajabu, wako watanzania ambao wanapata shida za kweli za kuunguliwa na moto lakini wanapopiga wanakuta simu (114) iko busy (inatumika) kumbe anayeitumia ni yule anayefanya masihara,"amesema Kamila

Mkazi wa Buhongwa jijini Mwanza, Ester Matiko amesema tabia ya watu kupiga simu wakiomba kujiunga Freemason inachangiwa na ugumu wa maisha huku akiwataka kuachana na tabia hiyo.

“Kuna uwezekano baadhi ya majanga hasa ya moto yangeweza kuzuilika lakini kwa kutokana na watu wa aina hii, baadhi ya familia zimepoteza mali na wapendwa wao kutokana na maofisa wa Zimamoto kuchelewa kupata taarifa wakiwasiliza watu wa aina hiyo (wanaofanya kejeli),"amesema Ester

Naye, Hassan Juma ameliomba jeshi hilo kutofumbia macho watu wenye tabia hizo badala yake wawakamate kisha kuwachukulia hatua za kinidhamu kwa mujibu wa sheria.