Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanne wafariki, sita wajeruhiwa ajali ya gari Handeni

Muktasari:

  • Ajali iliyohusisha basi la abairia na gari dogo aina ya Toyota Noah imesababisha vifo vya watu watatu na majeruhi wanne waliopelekwa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya Handeni.

Handeni. Watu wanne wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya BM Coach kugongana na Toyota Noah katika eneo la Manga Wilaya ya Handeni, Mkoa wa Tanga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo jioni ya leo Ijumaa, Septemba 29, 2023 na kusema ilihusisha Noah na basi la Kampuni ya BM Coach ambalo lilikuwa likitokea Barabara ya Segera.

"… Kweli imetokea ajali watu wanne wamefariki dunia na wengine sita wamejeruhiwa katika eneo la Manga wilayani Handeni," amesema Kamanda Mchunguzi.

Mganga Mfawidhi Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya Handeni, Abdulmajid Makoye amekiri kupokea miili ya marehemu hao pamoja na majeruhi wengine sita ambao kutokana na majeruhi yao walisafirishwa.

Amewataja majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni Amina Zuberi (50) mkazi wa Lushoto, Badru Hinda (4) na Nicolaus Mahimu (32) wa Dar es Salam, Joseph Joachim (39), Mariam Hamis (23) mkazi wa Kwamsisi na majeruhi wa mwisho ni Mwinjuma Hemed (23) mkazi wa Kabuku.

 "Katika watu waliofariki wapo watoto wawili, mmoja wa miezi 9 na mwingine miaka mitatu ambapo mmoja amefia hapa hapa hospitali na mwingine amefia kwenye ajali pamoja na wanaume wengine wawili," amesema Dokta Makoye.