Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanandoa waangukiwa na ukuta wakiwa wamelala

Diwani wa Kata ya Nyamazugo Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza, Enock Sengerema akiwajulia hali wananchi wake Wiliamu John na Melesiana Hamuduni wakazi wa Kijiji cha Kijuka Kata ya Nyamazugo walionusurika kifo baada ya kudondokewa na ukuta wa nyumba wakiwa  wamelala na mkewe.  Picha na Daniel Makaka

Muktasari:

  • Mvua zinazoendelea kunyesha wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza zinaendelea kuleta madhara, ambapo katika Kijiji cha Kijuka ukuta wa nyumba umewaangikia na kuwajeruhi wanandoa waliokuwa walala ndani.

Sengerema. Wanandoa wawili mkoani Mwanza wamenusurika kifo baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba walipokuwa wamelala.

Wanandoa hao, Wiliamu John (65) na mkewe Melesiana Hamidu (63) ambao ni wakazi wa Kijiji cha Kijuka Kata Nyamazugo wilayani Sengereme Mkoa wa Mwanza wamekutwa na mkasa huo usiku wa kuamkia leo Jumatano Desemba 27, 2023.

Kutokana na majeraha waliyopata, wanandoa hao walikimbizwa katika hospitali teule ya wilaya hiyo katika chumba cha dharura wanakopatiwa matibabu.

"Tumewapokea asubuhii ya leo na hali zao hazikuwa nzuri, tunaendelea kuwapatia matibabu na hali zao zinaendelea vizuri,” amesema Ofisa tabibu wa zamu katika hospitali hiyo, Dk Kephlen Kaswahili.

Akieleza tukio hilo hospitalini hapo, Melesiana ameelaza kuwa saa 5:30 alitoka nje kwenda hajandogo huku mvua ikiwa inanyesha alimwacha mume akiwa amelala na baada ya kurejea ndani, alisikia kama kishindo nje lakini aliendelea kulala.

Alisema baada ya dakika kadhaa wakiwa wamelala na mumewe wakaangukiwa na ukuta uliowafunika.

Naye John amewashukuru wananchi waliofika kuwasaidia maana walikuwa wamepoteza mweleko wasijue la kufanya baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba yao ya tope.

"Licha ya kuwa na maumivu ya kifua Nyonga ninaendelea vizuri nawashukuru madaktari walionisadia mimi na mke wangu,” amesema John.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Mwabasabi B Kijiji, Dotto Msula amesema baada kusikia kishindo alitoka nje na kukuta nyumba ya jirani yake imedondoka ndipo alipochukuwa jukumu la kuwaokoa, huku alipiga kelele wananchi walijaa na kufanikisha kuwaondoa kwenye kifusi.

"Baada ya kuwaokoa tulichukuwa pikipiki na kuwakimbiza Hospitali kwa ajili ya matibabu na kwa mjibu wa dakitari baada ya kuwa hudumia hali zao zinaendelea vizuri,” amesema Msula.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Nyamazugo Enock Sengerema ambaye amefika Hospitalini hapo kuwajulia hali majeruhi amewashukuru madaktari waliowahudumia kuonyesha moyo wa upendo.

Amesema kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa hapa nchini nyumba nyingi ambazo siyo imara zitaendelea kudodoka hivyo wananchi wanatakiwa kuchukuwa tahadhari juu hali hiyo.