Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu wanandoa kutembelea Ziwa Nyasa

Mkurugenzi wa kampuni ya Mc Edwin Luvanda  branding Entertainment, Edwin Luvanda akieleza lengo la wanandoa 800 kufanya utalii wa ndani mwambao kwa ufukwe wa ziwa Nyasa Mkoa wa Mbeya. Picha na Hawa Mathias

Muktasari:

  • Wanandoa 800 wanatarajiwa kufanya utalii wa ndani Ziwa Nyasa kwa lengo la kuwajenga kisaikolojia na kuweza kumudu mahusiano kwa kuepuka migogoro ambayo imekuwa ikisababisha madhara makubwa kwenye familia.

Mbeya. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limesema litaimarisha ulinzi katika ufukwe wa Ziwa Nyasa Wilaya ya Kyela mkoani hapa, kufuatia kuwepo kwa ugeni wa wanandoa 800 kutoka mikoa mbalimbali nchini kufanya utalii na kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo.

Mbali na kufanya utalii pia kutakuwepo na mada mbalimbali ikiwepo elimu ya kukabiliana na matukio ya ukatili wa kijinsia, wivu wa mapenzi, migogoro ya ndoa kwa lengo la kurejesha amani na maadili katika ngazi za familia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga ameliambia Mwananchi leo Jumatano, Oktoba 25,2023 ikiwa ni siku chache  kuelekea tukio hilo linalotarajia kufanyika Jumamosi Oktoba 28 mwaka huu.

“Nimepokea simu kutoka Mkurugenzi wa Kampuni ya MC Edwin Luvanda Branding and Entertainment kuwepo kwa tukio hilo kubwa ambalo litakutanisha wanadoa 800 kutoka mikoa mbalimbali nchini hiyo ni fursa pekee ambayo italeta matokeo makubwa ya kuvutia wawekezaji na watalii wa ndani na nje ya nchi,” amesema.

Amesema licha ya kufanya utalii pia masuala mbalimbali yatakuwepo ikiwepo kujadili namna bora ya kurejesha mahusiano ya wanandoa na lengo ni kuwarejesha kwenye maisha ya awali na kuondoa makwazo na changamoto zilizopita ili kupunguza visa, mauaji katika kundi hilo.

“Mwenyezi Mungu akinijalia nitaweza kushiriki kwani elimu ya ukatili wa kijinsia, migogoro ya ndoa, mauaji kwa sasa nipo kwenye ziara maeneo mbalimbali kutoa elimu ili kuhakikisha jamii inakuwa na uelewa mpaka kwa lengo la kuyapunguza au kuacha kabisa,” amesema.

Mkurugenzi wa Kampuni ya MC Edwin Luvanda Branding and Entertainment, Edwin Luvanda amesema kuwa lengo kubwa ni kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza utalii wa ndani na kuvutia wawekezaji katika ufukwe wa Ziwa Nyasa.

“Huwa tunaandaa matukio mbalimbali hususani kwa walio kwenye ndoa na wasio kwenye ndoa lengo kuwajenga kisaikolojia na kuweza kumudu mahusiano kwa kuepuka migogoro ambayo imekuwa ikisababisha madhara makubwa kwenye familia,” amesema Luvanda.

Ametaja faida za ushiriki wa wanandoa ni kudumisha amani na upendo huku akieleza kupitia kundi hilo la watu 800 Serikali itarajie kupokea wawekezaji wengi wa ndani na nje ya nchi na kuchangia kuongeza mapato ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais Samia katika kutangaza vivutio vya utalii wa ndani.

Rebecca Kinyunyu ambaye ni mshiriki wa tukio hilo amesema ni fursa pekee ambayo inaonyesha nia ya dhati kwa Watanzania kufanya lile tamanio la kiongozi Mkuu wa nchi kuwekeza kutangaza utalii wa ndani.

“Mkoa wa Mbeya una fursa nyingi za utalii ambazo zikitangazwa kuna uwezekano mkubwa wa kuvutia wawekezaji wengi na kwamba ni wakati sasa Serikali kuunga mkono wadau wanaojitoa kutangaza fursa hizo,” amesema.