Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wananchi: Kuhama Ngorongoro ni hiari, wanaobaki wasinyanyaswe

Muktasari:

 Baadhi ya wakazi wanaohama katika Hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha wameiomba serikali kutowanyanyasa wanaobaki hifadhini kwa kuwa kuhama ni hiari.



Arusha. Baadhi ya wakazi wanaohama katika Hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha wameiomba serikali kutowanyanyasa wanaobaki hifadhini kwa kuwa kuhama ni hiari.

Ombi hilo limetolewa leo Alhamisi Januari 12,2023 katika shughuli ya kuliaga  kundi la 17 la wakazi waliokuwa wanaishi ndani hifadhi wanaohamia eneo jingine.

"Sisi tumeamua kuhama kwa hiari yetu wenyewe lakini ombi letu tunaiomba serikali kupitia uongozi wa hifadhi ya Ngorongoro msiwanyanyase wanaobaki kwani zoezi ili linafanyika bila kushurutishwa," amesema Agustino Bajuta mmoja wa wakazi  wanaohama.

Naibu Kamishna wa uhifadhi, Dk Christopher Timbuka amesema kundi hilo la 17 lina jumla ya kaya 34 na watu w 179 ambao wameamua kuhamia Msomera mkoani Tanga huku wanne kati yao wakihamia mkoa wa Tabora.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro,  Raymond Mangwala amesema kitendo cha kuhama kwa hiari ni uzalendo kwani imefuata misingi yote ya utawala bora na haki za binadamu ili kudumisha amani ya nchi na kila mmoja anayeishi nchini.

Imeandikwa na

Teddy Kilanga, Mwananchi