Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanahabari, wananchi wazalisha maudhui kurudishwa ‘darasani’

Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Kiraia ya Jamii Africa Maxence Melo wa kwanza (kushoto) katika uzinduzi wa Jina Jipya la asasi hiyo ambayo zamani iliitwa (Jamii Forums), pamoja na Mpango Mkakati wa Miaka mitano. Picha na Sunday George

Muktasari:

  • Asasi ya Kiraia ya Jamiiafrica (Zamani JamiiForums), imekuja na mikakati kuwajengea uwezo waandishi na vyombo vya habari katika kuzalisha maudhui ya ndani ya nchi.

Dar es Salaam. Kutokana na ukuaji wa kasi wa teknolojia na mabadiliko katika jukwaa la sekta ya habari, waandishi wa habari na wazalishaji maudhui, wametakiwa kujengewa uwezo wa namna ya utendaji wa kazi hiyo.

Hatua hiyo inakuja kwa kuwa maudhui yanayozalishwa yanapaswa kutumika kumsaidia mwananchi mlaji katika kufanya uamuzi sahihi wa lipi alifanye.

Hayo yamejiri baada ya Asasi ya Kiraia ya JamiiAfrica kuja na mpango mkakati wa miaka mitano kuanzia 2025 hadi 2030 utakaokuza uwezo wa kuzalisha maudhui ya ndani yatakayoingia kwenye dijitali kusaidia wananchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiAfrica, Maxence Melo amesema katika mpango huo, wanajenga mifumo ya kisasa ya Kiafrika inayojali asili ya ilikotoka yenye masilahi kwa umma. 

Ameyasema hayo leo Aprili 24, 2025 katika uzinduzi wa jina jipya la JamiiAfrica lililobadilika kutoka JamiiForums hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Melo amesema wanafanya hivyo kwenye vyombo vya habari, waandishi na wananchi wazalishaji wa maudhui hayo ya asili.

"Takwimu za watumiaji wa huduma ya Intaneti kwa mwaka huu 2025 wamefikia milioni 50 kutoka milioni 25 mwaka 2020,  hivyo tukaona tusije na mbinu zilezile tushirikishe wadau mbalimbali ndani na nje ya nchi kujengea uwezo," amesema.

Melo amesema pia, mkakati unahusisha kushirikisha wadau wa Serikali ili kuwajengea uwezo pamoja na wananchi katika masuala ya utawala bora, uwajibikaji na hata demokrasia.

"Mkakati wa nne, unahusu ustahimilivu wa kidijitali, usalama pamoja na ushirikishwaji wa kidijitali utakaokuja na vifaa vyenye maudhui ya ndani ya asili.

Akizungumzia sababu ya kubadili jina Melo amesema ni baada ya kushirikisha wadau wakiwemo asasi za kiraia, mamlaka za nchi, nchi za Kenya, Rwanda, Uganda, DRC Congo, Uganda, Zimbabwe, Afrika Kusini ili kuhakikisha wanachokuja nacho kinatatua changamoto zilizopo Tanzania na nje ya nchi kwa kuja na mbinu mpya.

"Kwa maana hiyo tuko hatua za mwisho kuanzisha jukwaa jipya ifikapo Mei mwaka huu litakalohudumia wananchi wa nchi hizo katika kufanya maamuzi sahihi.

Akizungumzia mafunzo waliyotoa amesema wamekuwa na mafunzo maalumu kwa ajili ya waandishi zaidi ya 1,000 sasa wanaenda nje ya mipaka ya Tanzania.

Amesema; “katika ulimwengu huu wa kidijitali tuendelee kutoa mafunzo ili dijitali iendelee kuwa fursa na si tishio.”

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania, Kenneth Simbaya amesema waandishi wanachakata habari nyingi zikiwamo za mikoa ambazo zinaweza kuwa na masilahi mapana kwa Afrika nzima.

Amesema habari za ndani zinaweza kuwa za kibara hivyo waandishi wanapaswa kupanuka kutoka kufikiria kuripoti kwa kutumia jukwaa salama la kidijitali.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Melo amesema kwa upande wa sera na sheria za sekta ya habari, wataendelea kuhakikisha zinakua rafiki katika maeneo ya uchakataji wa taarifa.