Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uhuru wa vyombo vya habari watiliwa shaka Pakistan

Kamatakamata ya waandishi wa habari nchini Pakistan huku  baadhi wakiwekewa vikwazo kumeibua hali ya wasiwasi nchini humo kuhusu uhuru wa vyombo vya habari.

Baadhi ya wanahabari waliokamatwa na  watu wasiojulikana wakiwa wameficha nyuso zao na baadhi yao kufunguliwa mashtaka ya ugaidi ni Muhammad Waheed Murad wa gazeti la Urdu News na mwanzilishi wa jukwaa la habari la kidijitali la Raftar, Farhan Mallick.

Wadau mbalimbali wa habari kando ya kukosoa ukamataji huo wa wanahabari, walisema chanzo ni kasoro zilizopo katika Sheria ya Kuzuia Uhalifu wa Kielektroniki chini ya marekebisho yake ya mwaka 2025, wakidai kuwa ina vifungu vinavyombana zaidi mwandishi wa habari.

‘’Chini ya Sheria ya PECA, waandishi wa habari wanaoandika habari kuhusu masuala nyeti hasa yanayoihusu serikali wanakuwa katika wakati mgumu zaidi maana sheria haiwalindi. Yaani baadhi ya vifungu vinaweza kufafanuliwa kama habari husika ni ya uongo,’’ alisema mmoja wa wadau wa habari nchini Pakistan.

Tume ya Haki za Kibinadamu ya Pakistani (HRCP) imelaani vikali matukio hayo na kuyataja kuwa mashambulizi ya moja kwa moja dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari.

Pia muungano wa shirikisho la waandishi wa habari wa Pakistan pia umeelezea wasiwasi wake ukionya kwamba vitendo hivyo vinatishia msingi wa demokrasia.