Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ripoti Unicef yaitaja Pakistan

Muktasari:

  • Hali hii inadhihirisha jinsi ambavyo mabadiliko ya tabianchi siyo tu tatizo la mazingira, bali ni changamoto kubwa ya kijamii na kiuchumi, hasa kwa mataifa yanayoendelea kama Pakistan.

Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (Unicef) imeitaja nchi ya Pakistan kuwa miongoni mwa mataifa barani Asia yaliyo hatarini kukabiliwa na mabadiliko ya hali ya hewa huku watoto wakitajwa kuwa wataathirika zaidi.

Pakistan imekuwa ikikabiliwa na hali mbaya ya hewa, ikiwa ni pamoja na mafuriko makubwa, ukame, na viwango vya juu vya uchafuzi wa hewa, hali ambayo inawaweka watoto katika hatari kubwa ya maradhi, utapiamlo, na ukosefu wa elimu. 

Aidha, ripoti hiyo imebainisha kuwa kutakuwa na mafuriko, ukame na hali mbaya ya hewa katika baadhi ya maeneo nchini humo huku ikiitaka serikali kuweka mikakati kukabiliana na hali hiyo.

Mwaka 2022 nchi hiyo ilikumbwa na mafuriko yaliyoathiri zaidi ya watu milioni 33 wakiwemo watoto milioni 16.

‘’Watoto nchini Pakistan wapo hatarini kwa kuwa kwa sasa nchi hiyo inakabiliana na utapiamlo lakini pia inapambana kuboresha huduma za afya. Mabadiliko haya ya hali ya hewa yanaweza kuleta athari zaidi, hivyo ni vyema kujipanga mapema.’’

‘’Inatakiwa kuweka kipaumbele kwa sasa katika sera zake za hali ya hewa zinazozingatia mtoto, kuongeza ufadhili katika masuala ya hali ya hewa na kuzingatia mikakati ya kujiandaa na maafa,’’ inaeleza sehemu ya ripoti hiyo.

Ripoti hiyo pia imeyataja mafuriko ya mwaka 2010 nchini humo yaliyoathiri zaidi ya watu milioni 20, ‘’mafuriko hayo hayajasahaulika, kuna kitu serikali inatakiwa kufanya ili kuokoa kundi kubwa la wananchi hasa watoto.’’

‘’Tayari nchi inakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji na mabadiliko ya hali ya hewa yanaweza kupunguza upatikanaji wa maji. Hii inaweza kuwa na athari kubwa katika kilimo, viwanda.’’

Hata hivyo, ripoti hiyo inasisitiza kuwa watoto ni waathirika wakubwa wa mabadiliko ya tabianchi kwa sababu miili yao ni dhaifu zaidi dhidi ya magonjwa yanayohusiana na hali mbaya ya hewa, kama vile magonjwa ya njia ya upumuaji na magonjwa ya kuhara yanayosababishwa na maji machafu.