Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wamiliki wa vyombo vya habari kutoka nje wabanwa kisheria

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye

Muktasari:

Kanuni hizo zimeeleza kuwa mmiliki wa nje akitaka kuomba leseni kwa Mkurugenzi wa Idara za Huduma ya Habari atatakiwa kuorodhesha wamiliki wenza wa ndani ambao atashirikiana nao watakaokuwa na hisa zisizopungua asilimia 51.

Dar es Salaam. Baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kutangaza Januari 5 kuwa Sheria ya Huduma kwa Vyombo vya Habari iliyosainiwa na Rais John Magufuli, Novemba 2016 imeanza kazi mwanzoni mwa mwaka huu, kanuni zimeainisha baadhi ya mambo huku zikiwabana wawekezaji kutoka nje kuwa na asilimia 49 za umiliki wa gazeti.

Kanuni hizo zimeeleza kuwa mmiliki wa nje akitaka kuomba leseni kwa Mkurugenzi wa Idara za Huduma ya Habari atatakiwa kuorodhesha wamiliki wenza wa ndani ambao atashirikiana nao watakaokuwa na hisa zisizopungua asilimia 51.

Pia, mmiliki mmoja au kikundi cha watu ambao ni wazawa kanuni hazijaweka mipaka ya hisa wanazotakiwa kuwa nazo katika umiliki wa kampuni ya gazeti. Kanuni hizo zinaunga mkono Sera ya Habari ya mwaka 2013 na Sheria ya Huduma ya Utangazaji ya mwaka 1993 ambayo inamtaka mmiliki wa chombo cha habari kutoka nje asizidi asilimia 49 za umiliki wake.