Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakulima wa matunda na mbogamboga kicheko

Mkurugenzi wa TAHA, Dk Jacqueline Mkindi akizungumza katika mkutano wa kuboresha viwango vya ubora wa mazao ya mbogamboga na matunda. Picha Mussa Juma

Muktasari:

Tanzania inazalisha tani 47,000 za parachichi kwa mwaka, ambapo na tani 12,000 zinauzwa nje.

Arusha. Wakulima wa mbogamboga na matunda sasa wataweza kuuza bidhaa zao katika masoko ya kimataifa bila vikwazo baada ya kuanzishwa kwa taasisi ya kutoa ithibati ya ubora wa mazao katika masoko ya kimataifa.

Gharama za kupata ithibati ya kuwezesha kuuza nje mazao hayo zimepungua kutoka dola 6,500 na 7,000 hadi kufikia dola 3,000 na dola 3500.

Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya wakulima wa mbogamboga na matunda (TAHA), Jacqueline Mkindi ametoa taarifa hiyo leo Novemba 28, 2022 katika mkutano wa kimataifa wa Global GAP Tour Tanzania unaolenga kuboresha viwango vya uzalishaji wa mazao kwa ajili ya masoko ya kimataifa.

Mkindi amesema TAHA kwa kushirikiana na wahisani wa sekta ya kilimo imeweza kuanzisha taasisi ya Greencert Limited ambayo itakuwa ikisimamia ubora wa viwango vinavyohitajika katika soko la kimataifa.

Amesema wakulima nchini sasa wataweza kusaidia usalama wa chakula na viwango katila sekta ya Matunda na Mbogamboga.

Akizungumzia kukua kwa sekta ya kilimo hicho Mkindi amesema mafanikio ya sekta hiyo yametokana na jitihada za Rais Samia Suluhu kuwasaidia kupata masoko ya nje na kuboresha Mazingira ya kilimo.

Amesema soko la parachichi kutoka Tanzania limeongezeka na Tanzania itaanza kuuza nchi ya China yenye watu zaidi ya 1.4 billion soko kitakuwa kubwa zaidi.


"Ifikapo mwaka 2026 tunatarajia kuuza parachichi China ya thamani ya zaidi ya dola 96 milioni," amesema.

Kwa sasa Tanzania inazalisha tani 47,000 kwa mwaka huku tani 12,000 zinauzwa nje ya nchi.

Awali akifungua mkutano huo, Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde amesema Serikali kwa kushiriana na wadau imepanga kuikuza sekta ya kilimo cha mbogamboga na matunda kutoka dola 780 milioni kwa sasa hadi dola 2 bilioni mwaka 2030.

Mavunde amesema, katika soko la China tayari Rais Samia Suluhu alifanikisha kusainiwa makubaliano ya kuuza parachichi nchini China na hivi karibuni zao hilo litaanza kusafirisha.

"Lakini pia hivi karibuni tulikuwa na mazungumzo na Marekani ambapo tunakamilisha taratibu za kuanza kuuza parachichi nchini Marekani," amesema


Amesema tayari pia Tanzania imepata masoko ya parachichi katika nchi za India,Hispania na Afrika Kisini .

"Ili kuhakikisha tunazalisha mazao haya kwa wingi na ubora serikali inaendelea kuboresha mazingira ya kilimo hicho na inatarajiwa kutoa mbegu za Ruzuku za parachichi bora Miche 20 milioni," amesema

Alisema pia serikali inakusudia kujenga vituo vitatu vya mfumo wa mnyororo wa ubaridi ili kuhakikisha mazao ya mbogamboga na matunda yanayozalishwa yanahifadhiwa vizuri hadi kusafirishwa nje ya nchi.

Akizungumza katika mkutano huo mkulima wa Parachichi, Cosmas Kidiga wa Rungwe mkoani Mbeya ameeleza kupatikana masoko mapya kutasaidia kuongeza uzalishaji na kipato zaidi kwao wakulima.


"Mimi ninamiliki heka Tano natarajia kuongeza uzalishaji kwani Sasa tuna masoko mengi ya kimataifa"amsema.

Mkutano huo umedhaminiwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Ubalozi wa Finland, Shirika la Misaada la Marekani (USAID) taasisi ya Global GAP, Trade Mark East Africa, Trians, Agricord na Taasisi za USDA na FFD.