Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waitara aamriwa kumlipa Maswi Sh6 bilioni kwa kumkashfu

New Content Item (1)

Muktasari:

  • Katika kesi namba 23 ya mwaka 2023, Maswi aliwasilisha madai dhidi ya Mwita Waitara, Karoli Jacob na Mara TV, akiwataka wamlipe jumla ya Sh13 bilioni kama fidia ya madhara ya kashfa na tuhuma za uongo walizotoa dhidi yake kuhusu wizi wa fedha. Mahakama, baada ya kusikiliza hoja za pande zote, imeamuru wadaiwa wamlipe Maswi Sh6 bilioni kama fidia pamoja na kuomba msamaha kupitia vyombo vya habari nchini.

Musoma. Mahakama Kuu Kanda ya Musoma imemuamuru mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara pamoja na wenzake wawili kumlipa fidia ya Sh6 bilioni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Eliakim Maswi baada ya kupatikana na hatia katika kesi ya kashfa dhidi yao.

Hukumu hiyo ilitolewa mahakamani hapo jana Juni 16, 2025 na Jaji Marlin Komba ambaye amesema kwa mujibu wa ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo, amejiridhisha pasipo na shaka kuwa wadaiwa walitenda kosa hilo kinyume cha sheria.

Jaji Komba amewahukumu wadaiwa kumlipa Maswi Sh1 bilioni kama fidia ya  adhabu ya udhalilishaji baada ya kubainika kuwa alitumia maneno ya uongo na kumkashifu Maswi.

Pia, Jaji Komba ameamuru Maswi alipwe Sh5 bilioni kama fidia ya madhara ya jumla pamoja na kuombwa radhi hadharani kupitia vyombo vya habari.

Amesema kabla ya hukumu hiyo wadaiwa walitakiwa kuomba msamaha, lakini walikataa kufanya hivyo.

Jaji Komba amesema maneno hayo ya Waitara hayakuwa ya kashfa kwa Maswi pekee bali kwa watumishi wa umma kwa ujumla na kuwa Waitara aliamua kufanya hivyo kwa sababu hajawahi kuwa mtumishi wa umma.

Katika kesi hiyo, Maswi alidai kuwa Agosti 9, 2023, Waitara alitoa maneno ya kashfa dhidi yake katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Mtana, Kata ya Manga wilayani Tarime mkoani Mara, uliohudhuriwa na watu zaidi ya 500.

Alidai kuwa maneno hayo yaliandikwa na kuonyeshwa kupitia televisheni ya mtandaoni ya Mara TV kutoa maneno hayo yalikuwa ya uongo, yenye nia ovu, na yalilenga kushusha hadhi yake.  Katika kesi hiyo waliunganishwa Karoli Jacob na Mara TV.

Maswi alidai kuwa kwenye mkutano huo, Waitara alisema Maswi anahusika na kuwajibika kwa vitendo vya rushwa na matumizi mabaya ya nafasi yake kwenye utumishi wa umma, kama Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Ununuzi (PPRA).

Maswi alidai televisheni ya mtandaoni ya Mara TV ilichapisha maneno hayo na kwamba hadi Agosti 13, 2023 chapisho hilo lilitazamwa na watu zaidi ya 280 kutoka duniani kote.

Alidai kuwa maeneo hayo ya kashfa mbali na kuwa ni ya uongo na yenye nia ovu, yalilenga kumshushia hadhi yake katika jamii.

Machi 19, 2024 Mahakama hiyo ilimfungia Waitara na Jacob milango ya kujitetetea baada ya kushindwa kuwasilisha maelezo ya utetezi wa awali kwa njia ya maandishi kabla ya usikilizwaji wa kesi hiyo, uliokuwa unahitajika ndani ya siku 21.

Mahakama hiyo chini ya Jaji Komba ilifanya maamuzi hayo baada ya Waitara na mwenzake kutaka kuongezewa muda baada ya muda wa awali kuisha, ombi ambalo lilipingwa na Maswi kupitia wakili wake, Kassim Gilla.

Akitoa maamuzi hayo Haji Komba alikubaliana na pingamizi la upande wa mleta maombi akisema wadaiwa walipaswa kutoa sababu za kuridhisha za kuchelewa majibu yao, Machi 19, 2024 Mahakama hiyo ilimfungia Waitara na Jacob milango ya kujitetetea baada ya kushindwa kuwasilisha maelezo ya utetezi wa awali kwa njia ya maandishi kabla ya usikilizwaji wa kesi hiyo, uliokuwa unahitajika ndani ya siku 21.

Mahakama hiyo chini ya Jaji Komba ilifanya maamuzi hayo baada ya Waitara na mwenzake kutaka kuongezewa muda baada ya muda wa awali kuisha, ombi ambalo lilipingwa na Maswi kupitia wakili wake, Kassim Gilla.

Akitoa maamuzi hayo Haji Komba alikubaliana na pingamizi la upande wa mleta maombi akisema wadaiwa walipaswa kutoa sababu za kuridhisha za kuchelewa majibu yao,hivyo kesi inaendelea hadi mwisho na kutolewa hukumu.