Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wahasibu wanawake wahamasisha wanafunzi kupenda hesabu

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akizungumza kwenye kongaamano laa sita la Chama cha Wahasibu wanawake Tanzania (Tawc) lililofanyika jijini Mwanza. Picha na Saada Amir

Muktasari:

Chama cha wahasibu wanawake nchini (Tawc) kimetoa zaidi ya vitabu 5, 000 vya hisabati na biashara kwa baadhi ya shule za sekondari ikiwa ni kuwahamasisha wanafunzi kupenda masomo hayo.

Mwanza. Chama cha wahasibu wanawake nchini (Tawc) kimetoa zaidi ya vitabu 5, 000 vya hisabati na biashara kwa baadhi ya shule za sekondari ikiwa ni kuwahamasisha wanafunzi kupenda masomo hayo.

Akizungumza Agosti 16, 2023 kwenye kongamano la sita la wanawake na uongozi lililofanyika jijini Mwanza, Mkurugenzi Mtendaji wa Tawc, Tumaini Lawrence amesema vitabu hivyo vimetolewa shule mbili za Dar es Salaam na moja ya Zanzibar.

 “Tumeanzisha suala la kuwahamasisha wanafunzi wa kike na wakiume mashuleni kwa kuwapelekea vitabu vya hesabu, commerce na book keeping  pamoja na kuwahamasisha kwamba sisi tulifanya vizuri kwenye mambo ya hesabu,

“Na wao tunawaomba waweze kufanya vizuri katika hesabu ili kuwajengea msingi mzuri wa kujifunza mambo ya hesabu mwisho wa siku tuendelee kuwa na idadi kubwa ya wahasibu,”amesema

Akizungumzia kogamano hilo, amesema mada kuu katika kongamano hilo ni ‘kiongozi bila cheo'ambapo watazungumzia nafasi ya mtu kuwa kiongozi pasipo ulazima wa cheo.

“Sio lazima cheo ndo mwanamke awe kiongozi bali ni kujiandaa tu popote ulipo na katika mazingira uliyonayo haijalishi unayo kazi au hauna lakini kikubwa ili uweze kuwa kiongozi ni uwe na tabia za uongozi hivyo tunamuandaa mwanamke aliyepo hapa ili awe kiongozi asisubili tu kuteuliwa au kuchaguliwa,”amesema Tumaini

Amesema tangu chama hicho kianzishwe mwaka 2015 kikiwa na wanachama 15 wamekuwa wakihamasisha wahasibu kujiunga nakufanikiwa kusajili wanachama zaidi ya 920 hadi sasa.

 “Jamii ilikua inajua kwamba mhasibu ni mtu tu anayekaa ofisini hivyo tangia tumeanzisha hiki chama tumeipinga kauli hiyo kwamba mhasibu siyo mtu tu ayekaa ofisi bali anaweza hata akaisaidia jamii vitu vingine kama kuifundisha kuhusiana elimu fedha na matumizi mazuri ya fedha,”amesema

Akitoa taarifa ya chama hicho, Mwenyekiti wa Tawc, Dk Neema Kiure amesema kongamano hilo pia limehusisha wanawake wa fani zingine lengo likiwa kujengeana uwezo katika kuongoza.

Naye, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akifungua kongamano hilo amesema wanawake wanapaswa kuwatia moyo wanawake wenzao kwa kuwafungua akili na kuwaonyesha fursa zinazohusiana na uongozi katika sekta mbalimbali.

"Tunatakiwa kufungua fursa kwa baadhi ya wanawake ili kujua majukumu yao kama wanawake na kuwapatia elimu wengine ambao hawana elimu kuhusiana kuijenga familia katika malezi bora na ya kidini pamoja na kuhamasisha sifa za kuwa kiongozi bora kwenye jamii,"

"Sisi wanawake inatakiwa tuguse maisha ya wanawake wengine na tubadili mtazamo kwa wanawake wenzetu ambao hawana elimu kuhusiana na uongozi katika jamii zetu zinazotuzunguka," amesema Waziri Mabula

Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo, akiwamo Jalia Mayanja kutoka Mfuko wa Mafao ya Jamii (PSSF) na Donasia Masambo ambaye ni mtaalam wa kodi wamesema wanawake wasisubiri kupata vyeo vikubwa vya kisiasa ndiyo wafanye mambo chanya bali wanatakiwa kupigania fursa za uongozi kuanzia ngazi ya chini kwenye vitengo mbalimbali.

“Nategemea baada ya mkutano huu nitaonyesha tofauti kwa wale walioko chini yangu lakini pia nimepata elimu mbalimbali kutoka kwa watoa mada ambao wametuasa tusibweteke katika jamii zetu bali tukapambane tujitengenezee vyanzo mbalimbali vya mapato na uwekezaji kukidhi mahitaji ya familia," amesema Jalia