Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wafanyabiashara wanaotumia Bandari ya Karema hii inawahusu

Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile akijibu maswali ya wabunge leo Mei 6, 2025 bungeni jijini Dodoma. Picha na Hamis Mniha

Muktasari:

  • Serikali imesema inaendelea na mazungumzo ya kitaalamu ili ianze ujenzi wa barabara kutoka Moba hadi Lubumbashi (DRC) ili kuwapunguzia usumbufu wa kupita Zambia wafanyabiashara wa Tanzania.

Dodoma. Mbunge wa Momba (CCM), Condester Sichalwe ameibana Serikali akitaka kujua ni lini itaanza ujenzi wa barabara Moba hadi Lubumbashi (DRC) ambayo amesema ni muhimu na tegemeo la wafanyabiashara.

Sichalwe leo Jumanne Mei 6, 2025 amehoji akitaka kujua mkakati gani unafanyika kwa makusudi ili kuondoa usumbufu ambao umekuwa ukiwapata wafanyabiashara wanapopitia Zambia, akisema imekuwa ni usumbufu mkubwa na kukatisha tamaa.

Kwenye swali la msingi amehoji kwa nini Serikali iliamua kujenga Bandari Karema wakati upande wa DRC bado hawajajenga.

Akijibu maswali hayo kwa pamoja, Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilisaini hati ya makubaliano.

Kihenzile amesema mkataba huo ulikuwa kwa ajili ya kuboresha na kuimarisha miundombinu ikiwemo bandari ili kuchochea shughuli za kiuchumi baina ya nchi hizo mbili.

“Katika kutimiza azma hiyo, Serikali kupitia TPA (Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania) ilianza maboresho ya Bandari za Kigoma pamoja na ujenzi wa Bandari mpya ya Karema katika Ziwa Tanganyika ili kusaidia kuchochea uchumi lakini kuwarahisishia na kuwaondolea usumbufu wafanyabiashara,” amesema Kihenzile.

Naibu Waziri amesema kwa sasa TPA inaendelea na kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa awali kwa ajili ya kuendeleza Bandari za Moba na Kalamie katika ziwa Tanganyika upande wa DRC.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri, mpango wa ujenzi wa barabara ya Moba hadi Lubumbushi walishaanza mazungumzo na wataalamu ili kuona namna wanavyoweza kufanya ili kuanza ujenzi wa barabara hiyo.