Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wafanyabiashara Soko Kuu Mwanjelwa wagoma

Hali ilivyo Soko Kuu la Mwanjelwa jijini Mbeya kufuatia mgomo wa wafanyabiashara kutofungua maduka kutoa huduma.

Muktasari:

  • Mgomo huo umeanza leo alfajiri, wafanyabiashara hao wamegoma kufungua maduka, huku wananchi wakikosa huduma.

Mbeya. Wafanyabiashara katika Soko Kuu la Mwanjelwa jijini Mbeya wamegoma kufungua maduka yao na kusababisha adha kwa wananchi ya kukosa huduma.

Mwananchi Digital imefika sokoni hapo leo Alhamisi Mei 23, 2024 na kushuhudia milango yote imefungwa huku baadhi ya wananchi waliofika kupata huduma wakiduwaa wasijue la kufanya.

Baadhi ya wafanyabiashara ambao wamegoma kurekodiwa wamesikika wakilalamikia kuumizwa na utitiri wa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na za Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

"Hatutafungua hadi tukipata muafaka wa hiki kinachoendelea, kodi ni nyingi, biashara yenyewe ni ngumu, tunafungiwa maduka kwa tozo nyingi, nyingine ziko nje” amedai mmoja wa wafanyabiashara hao.

Mwananchi inaendelea kuzitafuta mamlaka husika pamoja na uongozi wa soko hilo kujua hatima ya kurejea kwa huduma sokoni hapo.

Taarifa zaidi zinakujua endelea kufuatilia mitandao yetu ya kijamii.